
Wakati wa Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26
Aprili 1964, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa
Zanzibar Abeid Amaan Karume ambao sasa wote ni Marehemu, walipanda
katika shimo moja Miembe miwili mmoja kutoka Zanzibar na mwingine kutoka
Tanganyika. Miembe hiyo imekuwa na kustawi pamoja na kufanya shina moja
‘through grafting’. Mti huo wa mwembe umestawi vyema katika
bustani ya Ikulu, Dar es Salaam, kama unavyoonekana Aprili 26, 2014
ambayo ni Siku ya miaka 50 ya Muungano.
No comments:
Post a Comment