PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
SHIRIKA
la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Radio ya Kimataifa ya
Jamhuri ya Watu wa China (CRI) leo kwa pamoja yameshirikiana katika
sherehe ya Uzinduzi wa Tamthiliya ijulikanayo kwa jina la MAPENZI NA
FURAHA YA KIJANA (Jin Tai Lang) ambayo imechezwa na China na kuwekwa
sauti kwa lugha ya Kiswahili na wasanii wa Tanzania.
Sherehe
hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya TBC ikishuhudiwa na mgeni rasmi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Elisante Ole Gabriel akiwemo Mwakilishi wa Balozi toka Ubalozi wa China
nchini Tanzania, Wajumbe wa Bodi ya Wakaurugenzi TBC, Mkurugenzi Mkuu
Star Media Tanzania, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali na
wafanyakazi.
Hatua
ya uzinduzi wa sherehe hiyo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya
Serikali ya kujenga mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki kupitia
nyanja mbalimbali ikiwemo habari, Utamaduni na michezo.
“Pamoja
na kutekeleza sera za Serikali pia TBC tunatambua umuhimu wa kuwa na
michezo ya kuigiza ambayo inazingatia utamaduni wa Watanzania na
niwahakikishie kuwa Tamthiliya hizi zimeonesha hali hiyo.”. Alisema
Mkurugenzi Shirika la Habari Tanzania Clement Mshana.
Mashirika
ya habari ya TBC na CRI yamekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha
ushirkiano nah ii ni mara ya tatu kuwa na Tanmthiliya ya Kichina
iliyowekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili ambapo mwaka 2012 kulikuwa na
tamthiliya ya MAU DOU DOU NA VISA VYA MAMA WAKWE ZAKE, ikifuatiwa na
tamthiliya mbili nyingine ya MAISHA YA MAMA na FURAHA YA BABA ambazo
zote zimepata umaarufu.
Na: Benedict Liwenga
No comments:
Post a Comment