
Mshindi wa Tuzo za Msanii bora wa hip hop pamoja na Mwandishi bora wa mashairi ya HipHop KTMA 2014 Fid Q katika ngoma aliyoshirikishwa na Rapper JCB inayoitwa "Sina Muda" amemfokea Dayna kwa kutumia mkorogo unao badilisha ngozi yake na kuonekana mweupu hali ambayo Fid anadai kuwa Dayna anaukimbia uafrika, Mistari ya Verse hiyo inasomeka kama ifuatavyo:-
"Hi Dayna, sikufichi ulikua unahusika/
au mtoto wa uswazi ' akijichubua ' haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/

Kwa Upande wa Dayna Msanii, yeye nilikutana nae Ijumaa iliyopita pale Club Billicanas nikamdokeza kuhusu line ya Fid Q akanijibu kuwa hajawahi kuiskia wala kuambiwa so akaniahidi atai download ngoma hiyo aisikilize vizuri, Leo nilipomvutia wire Dayna akanijibu ameisikia na anamuheshimu Fid Q kwa wazo lake ila kwa wakati huu amepunguza kidogo kutumia mikorogo.
No comments:
Post a Comment