Huwa matukio kama haya au hisia kama
hizi sio rahisi kuonekana waziwazi kwa kiongozi wa nchi pale
anapohutubia au kuzungumza na Taifa kwa njia ya TV.
Imetokea kwa rais wa Korea Kaskazini
Park Geun-hye akilihutubia taifa kuhusu kivuko kilichozama April 16 2014
na kuua watu wapatao 300 huku wengi wao wakitajwa kuwa Wanafunzi ambapo
kwenye hii hotuba rais aliomba radhi kwa uzembe uliofanyika kwenye
vikosi vya uokoaji.
Jumapili iliyopita Rais huyu alihudhuria
ibada kanisani kuwaombea waliofariki kwenye ajali lakini pia alikutana
na ndugu waliopoteza watoto/ndugu zao kwenye kivuko hicho ambapo
waliozembea wanaadhibiwa sheria.
Miili 286 ilipatikana lakini mpaka sasa
18 haijaonekana, watu 172 wakiwemo 22 Wafanyakazi wa kivuko hicho kati
ya 29 walinusurika kwenye ajali hii.
Ukitaka kumuona rais mwenyewe akiongea kwa hisia na kutokwa machozi tazama hii video hapa chini
No comments:
Post a Comment