26 June, 2014

JACK PATRICK AFYA TETE GEREZANI

Unaweza kusema ni majanga juu ya majanga yanazidi kumkumba modo wa Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ baada ya wiki iliyopita kushindwa kupanda kortini kufuatia kutetereka kwa afya yake bila kufafanuliwa.
Mbali na kuwa na afya tete, pia Jack anadaiwa kulalamikia haki za msingi za kibinadamu ambazo anazikosa mahabusu kwa kuishi maisha kama ya mtu aliye kifungoni.
Akizungumza na gazeti pendwa la hapa Tanzania, mtu anayejitolea kumpa msaada na kumtembelea Jack mahabusu, Macau, China alikoshikiliwa, Matilda alisema Jack anaumia kwa kupewa maisha kama tayari amehukumiwa, anaona bora hukumu yake ipite ajue moja.
“Kiukweli Jack anaumwa, alishindwa hata kwenda mahamani, mbaya zaidi hata wakili wake naye hakutokea siku hiyo.
“Halafu kule mahabusu anafanyishwa kazi ngumu ambazo hastahili kama mahabusu na amesema hata watu wake wa karibu ambao anaamini kwa kipindi hiki wangekuwa wanampa faraja hawaoni, anatamani angekamatiwa Bongo labda kuna watu wanapenda kwenda kumtembelea kule Macau lakini hawana uwezo.
“Wabongo wengi ambao wako Macau kwa ajili ya sanaa ya sarakasi ndiyo kidogo wanakwenda kumtembelea siku mojamoja,” alisema Matilda.
Juni 20, mwaka huu, gazeti hilo lilizungumza na Mbongo Fleva anayedaiwa ni mtu wa karibu na Jack, Juma Khalid ‘Jux’ na kumuuliza kwa nini hajawahi kwenda kumtembelea ‘bebi’ wake mahabusu kama wanavyofanya Wabongo ambao wako Macau, hakuwa na majibu yaliyo nyooka



No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...