20 June, 2014

MASKINI FLORA! SOMA ALIVYO SHUSHULIWA BAADA YA KUTUPIA PICHA FB YENYE MANENO HAYA... AOMBA MAOMBI YA WATANZANIA!

Photo 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu ni nyepesi iliyo ya muda kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana. 2wakorintho4:16
 
 Maneno hayo aliyo post ikisindikizwa na picha hiyo iliwatibua watu na kuanza kumtiririkia soma baadhi tu ya yaliyoandikwa!
 
  • Augustino Faustine nikweli  hawa watu sina hakika kama walimshika mungu sawa sawa,roho mt hamwongozi mtu kutoa siri za ndani,wana paswa KUTUBU wote wametenda dhambi
  • Derrick Mbaku rudi kwa mume wako kwanza
  • Dorothea Andrew WAPENDWA UNAPOITAMBUA KWELI YA KRISTO NA UKAANGUKA ANGUKO LAKE SI DOGO MAANA SHETANI ATAKUKANDAMIZA HAPO CHINI. MWAMBIE YESU NIINUE NISIMAMISHE TAMBUENI KUSUDI LA MUNGU KATIKA MAISHA YENU HEBU UPOFU UWATOKE KWAJINA LA YESU MUONE NAMNA MUNGU ANAVYO WAWAZIA MEMA. MWAIBISHENI SHETANI KWA KURUDISHA MAHUSIANO YENU.KWANGUVU ZENU NI KAZI ILA KWA MSAADA WA MUNGU HAKUNA LISILO WEZEKANA KWAKE YEYE AAMINIE.
  • Prisca Mwabulanga We Angel John umeokoka kwajili ya nafsi yako au flora Mbasha! Kwani vichaa wangap umewaona barabarani wanaokota makopo mbona wewe huokoti kwasababu wao wanaokota jifunze kusimama kwa nafsi na kama wewe huna dhambi muombee aliye na dhambi asamehewe acha kumhukumu na kuandika maneno makali. Ni wajibu kuomba na kuwaombea watakatifu wote kama Paulo alivyosema kama Flora kaanguka ujue na wewe kama mkristo una nafasi kubwa ya kuwa umechangia katika hilo. Vita na mtu imeandikwa wapi dada, ninachojua vita yetu ni katika ulimwengu wa roho juu. Lia na Mungu wako anayekupa kutenda sawa ampe neema na Flora atende sawa kama unaona hayuko sawa.
  • Samwel Shamy dada inabidi ujitahidi mmalizane kwanza na mumeo vinginevyo watu wa mataifa ukiwahubiri watakuona kama msanii wa gospel na siyo mtumishi wa Mungu
  • Immanuel David Urio Mungu haruhusu kuachana. ni kusameana na kuendelea pamoja. na mrudi kanisa la mito ya baraka, hawa manabii na mitume wa sasa hivi watatupoteza

  • Elikana Nkwija Kama kweli mbasha kayafanya hayo basi mungu afanye yake na kama umemuxingizia basi adhabu utakayo ipata kwa mungu usije uxije ishangaa!!
  • Augustino Faustine hakuna huduma hapo mpaka ndoa itengamae,UKILETA SADAKA MADHABAHUNI NA HUKU UKIKUMBUKA KUWA NDUGU YAKO ANANENO JUU YAKO IACHE SADAKA YAKO MBELE YA MADHABAHU UENDE ZAKO UPATANE KWANZA NA NDUGU YAKO NDIPO URUDI KUTOA SADAKA YAKO.sadaka anayo itoa flora ni uimbaji sasa inakuwaje anaendelea kuimba huku ana neno na mume wake????????
  • Samwel Shamy Sophia Hebron hapa hakuna ku-keep going,kama flora anataka asionekane muhuni na kupitia huduma yake watu wamuone mungu basi aangalie alikoanguka,mimi nimesikiliza mahojiano yake vizuri yanaakisi chuki iliyokithiri kwa mumewe,yeye kama mtu wa mungu hata sasa ana uwezo wa ku-pre empty hili jambo wakalizungumzia nyumbani
  • Samwel Shamy biblia inasema mtu wa kwenu/mlokole akikosa basi sema naye na asipokuelewa waite wazee mzungumze lakini akishupaza shingo huyo ahesabiwe kama mtu wa mataifa/ ahukumiwe kisheria..........lakini maandiko yanasema hata watu wa mataifa hufanya hivi kwa kuwapenda marafiki zao na kuwachukia maadui zao,je mkifanya hivi mna tofauti gani na wa mataifa? ......via kuaibisha imani
  • Samwel Shamy Mungu wa mbinguni mara zote anatazama mzizi wa tatizo,huenda ikawa mzizi wa tatizo kwenye familia yako ni kipaji kizuri cha uimbaji aidha ni utanashati wa emma,lakini Mungu ili atibu tatizo atalaani kiini ili amani iwepo,KRISTO HAKUSHUGHULIKA NA SHINA LA MTINI/mafanikio yanayoleta kiburi bali alilaani mizizi na mtini ukanyauka
  • Augustino Faustine pia biblia inasema MKIUMANA MSIMALIZANE hawa wamesha malizana
  • Amani Nyakarashi KWA MTU WA KAWAIDA NI RAHISI TU, DEVORCE, ILA KWA WATU MNAOMTEGEMEA MUNGU, NA MLIOKIOO CHA JAMII, TUNASUBIRI JAMBO MOJA TU, "NIA NJEMA IDHIHIRIKE" MIONGONI MWENU, KATIKA JINA LA YESU. KAISARI NAYE TUMUACHIE AFANYE UCHUNGUZI, SIPENDI WALA HATUONI FAIDA YOYOTE KWA NDOA YENU KUVURUGIKA, MIMI NATAKA MUWEKE HISTORIA MRUDIANE, HALAFU ACHENI MAHAKAMA IFANYE UCHUNGUZI MPAKA MWISHO, SABABU ALIYESHITAKI NI BINTI SI FLORA MBASHA.
  • Augustino Faustine neno la mungu ni upanga ukatao kuwili sas injili inakukata mwenyewe

  • Obed Mwambene Umemkalibisha shetani katka ndoa yako alafu anatuletea mistar, hata sadaka yako saivi haiwez pokelewa na mungu had utakapo patana na mme wako
  • .

  • Regy Edward Usiangalie kibanzi kilichopo kwenye jicho la mwenzio wakati una boriti kubwa jichoni mwako, songa mbele Flora Mbasha, hata Daudi alimkosea Mungu lakini alijutia makosa yake na Mungu akamsamehe akamwita Daudi wewe ni jicho langu iweje leo kumbeza Mtumishi wa Mungu? Songa mbele tena mpende Mume wako sana usiangalie kilichotokea mwangalie shetani anayevuruga huduma yako umkemee.
  • Regy Edward Usimwangalie mwanadamu anasema nini we liangalie NENO linasema nini juu yako.
  • Prisca Yedidia Mcsam kama bado uko hotelini inabidi utoke huko haraka nyumba yako unamuachia nani? Mungu anakuangalia je ni hakima gani utatumia kama mwanamke kuokoa ndoa yako, cku zote nyumba ni mwanamke ndo anayeweza kuokoa ndoa yake isizame
    na cku zote unatakiwa ujue jicho la Mungu liko kwako anakutazama je unatakaje kuhusu hyo ndoa yako? kama huyo mume wako ulimpata kwa maombi inamaana umeacha kumuombea adui akapata nafasi, mbasha ni mume wako tu hatakaa awe wa mtu mwingine mpiganie mume wako kwa gharama yyte kiburi na kutokujishusha ndo kutasababisha aibu iendelee kukuandama.panda rank ktk Jina la Yesu sameaneni na mumeo ili shetani ajue hana kitu kwako.
  • Alpher Sospeter Bright wewe ni msanii wa nyimbo za injili, huna utumishi wowote wa MUNGU, kagombee ubunge CCM,
  • Javan Chela msalimie Gwajima

  • Masubi Bulula amen, jiepushe na dharau, uongo, usengenyaji n.k ili umtumikie Mungu salama. Mungu anahitaji vijana wenye nguvu kama wewe ili kazi yake einde. Epuka kukimbilia ktk magazeti kupeleka mambo yenu ya ndani
  • Tond Lameck PATANA TU KWANZA NA MMEO HARAFU UTAKUJA UONGEE MENGI TU HAPA FB. Injiri huwa haiendi hivi, hautaeleweka dada.

  • Samwel Shamy Mambo mengine yako ndani ya uwezo wetu wala mungu ahitajiki. Mfano kujishusha na kufanya compromise yakaisha
  • Munga Ibrahim Mchengwa Tubuni maana ufalme wa Mungu umekariba
  • Baraka Komba wala huna haja ya kujibizana na wanadamu maana sio adui zako utapoteza muda ingia kwenye chumba chako cha siri na Mungu wako aonae sirini ataweka mambo sawa

  • Sariaely Kaaya Pole xana ndo safari ilivyo tayar unao ushindi kaza kiatu, km nguo zako zimelegea hebu angalia Efeso 6:

  • Mugabe Mwangoka Kumbuka vita vyetu si vya damu na nyama japo majaribu yanachoma kama moto lakini majaribu ni mtaji....
  • Ngazagu Mwakilishi KAMWE MUNGU HAMWACHI MTUMISHI WAKE ASHINDWE NA SHETANI BALI UMPIGANIA. KUMBUKA MUNGU AKIWA UPANDE WETU HAKUNA WA KUSHINDANA NASI. MAKWAZO AYANA BUDI KUJA LAKINI OLE MTU YULE AYALETAYO.
  • Baraka Masaba Vita ni vikali shetani halali,Tunapigana ili hata tukifa tufe ktk Kristo,Kuna maisha baada ya kifo,Na kuna sehemu 2 za kwenda Baada ya kifo ili kusubilia Palapanda,(Kuzimu/Paradiso,)Mara nyingi moyo hautambui hii siri,Lkn roho inajuwa,Sasa Amani ndo huchagua,Ukiwa na Amani ya moyo kila kitu utakishinda,Shetani mjanja sana ukicheza tu umeumia,,,,Mara nyingi tatzo linapokuja huwa chanzo kiko mwanzo wa tatzo,Mwili huu hata ukifa wenyewe hauna hasara maana vumbini ndo nyumbani kwake ila roho yako yani wewe ndo inabeba dhamana ya Matatzo au Mafanikio yako,Kiroho/kimwili,Tatzo halimalizwi na tatzo isipokuwa vikikutana vinazaa tatzo ndugu yao mwingine,Hata ufanye nini tatzo halimalizwi na tatzo....Ukiishi kwa kutegemea fanikio fulani ujuwe tatzo anasubilia nafasi yake,,,,Tuishi maisha ya tukijuwa hata ukifa unaishi.....Mungu awabariki....METHALI
     
    Na dakika chache zilizopita Flora ame tupia tena post yenye akisisitiza watu wamuombee!!

    Kama unaweza kushiriki maombi haya pamoja nami, Mungu akukumbuke, na kama upo kwa ajili ya kuhukumu, pia Mungu akukumbuke. Math7:1 Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi, kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayo hukumiwa; na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakacho pimiwa.
    Math5:44 Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.

    ' Mungu wewe ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. wewe ni Mkuu sana, wewe ni mwanzo tena mwisho zaidi yako hakuna na hatakuwepo. umesema ktk 1wathesalonike5:18 shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu ktk kristo Yesu. ahsante Mungu maana wewe uliijua jana yangu, leo na kesho itakuwaje.Mungu wa amani unitakase kabisa nafsi yangu, mwili wangu na roho yangu unihifadhi, wewe BWANA ni mwaminifu.
    Ktk Isaya43;19 umesema,Tazama nitatenda neno jipya: sasa litachipuka je hamtalijua sasa? nitafanya njia hata jangwani na miito ya maji nyikani. BWANA mapenzi yako yatimizwe, tenda lililo kusudi lako juu yangu. ktk Math14:14 umesema, mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya. ukasema ktk Marko10:27 Yesu akawakazia macho akasema, kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo: maana yote yanawezekana kwa Mungu.

    Maombolezo3:31-32 Kwa kuwa BWANA hatamtupa mtu hata milele, maana ajapo mhuzunisha atamrehemu kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
    Mungu inua moyo wangu sasa, wewe ndiyo msaada pekee wa kweli. Ninaamini utatenda makuu kama ilivyoandikwa ktk Zaburi 108;13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, maana yeye atawakanyaga watesi wetu. Bwana wewe ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lako,pigana sasa ninakuachia wewe.

    ninashuka mbele zako ninaungana na wenye uhai wanne ktk Ufunuo4;6-11 kukuabudu wewe nikisema, 11 Umestahili wewe BWANA wetu na MUNGU wetu,kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako navyo vikaumbwa.
    Zab23;4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami.
    AMEN

     
     
 

 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...