21 June, 2014

VIONGOZI WA A.C.T WAPATA AJALI MOROGORO


Viongozi waandamizi wa ACT-Tanzania wapata ajali Morogoro
KIONGOZI wa chama cha siasa cha ACT Tanzania Bw Samson Mwigamba na wenzake kadhaa wamenusulika baada ya gari walilokuwa wakisafilia kuacha njia maeneo ya PANDAMBILI barabara ya Moro - Dom na kuanguka. Wote waliokuwamo ndani ya Gari wamepona na baada ya kushughulikia taratibu za kipolisi wataendelea na safari.
Wamo ziarani kuimarisha chama ambapo wanatarajiwa kuwa na mikutano katika Mkoa wa Kigoma kuanzia mwisho wa wiki hii. Nitawaletea habari kamaili kadri ninavyopata habari kutoka chanzo cha habari hizi.
MUNGU IBARIKI ACT TANZANIA MUNGU WAEPUSHE VIONGOZI NA BALAA ZOZOTE ZILE AMEN
============================== =====
By ACT-Tanzania Uenezi
Ndugu wana JF wapenzi wa ACT-Tanzania na watanzania wote kwa ujumla, ni Kweli kwamba Viongozi wa ACT-Tanzania akiwemo Katibu mkuu (wa muda) Ndugu Samson Mwigamba Katibu wa mawasiliano na Uenezi ndugu Mohamed Massaga na watu wengine wawili wamepata ajali Mbaya ya gari dogo wakiwa njiani kuelekea Kanda ya Magharibi kwa ajili ya shughuli za chama ambapo walikusudia kufanya Mikutano ya hadhara Katavi,Mpanda, Kibondo na maeneo mengine.
Tunamshukuru Mungu kwani wote wamenusurika katika ajali hiyo licha ya gari walilokuwa wakisafiria kuharibika vibaya.Tutumie fursa hii Kusaidia katika kuwasihi wasafiri wote wawe wanafunga mikanda kwa ajili ya usalama wao kwani inasaidia sana pindi ajali inapotokea.
Tutawapa habari zaidi kwa kadiri.
Source: JF

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...