MGANGA mmoja
wa jadi, hivi karibuni alikusanya umati mkubwa wa watu baada ya
kuinywesha dawa familia nzima ya mwanamke aliyemleta kwa lengo la
kumfanyia uganga ili kumrejesha mtoto wake aliyepotea katika mazingira
ya kutatanisha mjini Morogoro
Mwajuma
Bakari Tindwa mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Mwembesongo aliyemleta
mganga akiandaliwa dawa ili kumrejesha mtoto aliyepotea.
Tukio
hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita baada ya Mwajuma Bakari
Tindwa mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Mwembesongo kumleta mganga
huyo, Omar Ally ili amrudishe mtoto Omar Abdul Matenda (10), mwanafunzi
wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Uhuru, aliyepotea Juni 8, mwaka
huu.
…Bi. Mwajuma Bakari Tindwa akinywa dawa hiyo.
Mwajuma
alisema kuwa mwanaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kwa
zaidi ya wiki tatu, wamekuwa wakimtafuta bila mafanikio.
“Baada
ya kumkosa kote huko nilitoa ripoti Kituo cha Polisi Msamvu na kituo
kikuu cha polisi nao wamehangaika bila mafanikio, baada ya kujadiliana
na familia yangu tuliamua kumchukua huyu mganga ambaye alituhakikishia
kumrejesha mwanangu,” alisema.
Alipotakiwa
kuzungumzia mazingira ya mtoto huyo kupotea, alisema alikuwa akicheza
na mwenzake ambaye pia anaitwa Omar, lakini mwenzake alirudi na kudai
rafikiye amepotea kiajabu.
Mganga
huyo aliyefika hapo akiwa na timu ya watu wanne, alisababisha umati wa
watu kujaa kushuhudia alichokuwa akikifanya, ikiwa ni pamoja na
kumchinja paka na kuinywa damu yake, kuchimba shimo mithili ya kaburi
nje ya nyumba na kufukia msalaba.
…Timu nzima ya waganga waliofika kutoa huduma kwa Bi. Mwajuma Bakari Tindwa ili kumrejesha mtoto aliyepotea.
Aidha,
akitumia kifaa kama darubini, alimulika na kwenda nyuma ya nyumba
ambako alichimba na kutoa mapembe mawili, vitu ambavyo hata hivyo,
havikuwezesha kurejea kwa mtoto huyo.
Sangoma hao wakiwa na picha za maraisi wa awamu zote tatu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Tulipofika
hapa mtoto alikuwa jirani kwa mujibu wa vifaa vyangu, lakini sasa
wamempeleka umbali wa mita 250 hivyo kwa sasa tunaingia ndani na kufanya
shughuli zetu kwenye nyumba hii na baadaye tutaendelea na kazi ya
kumrejesha,” alisema mganga huyo baada ya kuona sura za watu zikiwa kama
zinazouliza.
Mganga akifanya vitu vyake kwenye shimo alilochimba nyuma ya nyumba.
Katika
hali ya kushangaza, mganga huyo alikutwa akiwa na picha za marais
watatu wastaafu, Baba wa Taifa na Ali Hassan Mwinyi sambamba na ya Rais
Jakaya Kikwete. Hadi gazeti pendwa (Uwazi) linaondoka eneo la tukio, mtoto Omar hakuwa
amepatikana.
Credit GPL
No comments:
Post a Comment