Mgoni, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) aliyefumaniwa akiwa na mke wa mtu
AMA kweli duniani kuna vituko! Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.
Ilibidi OFM itie timu kwenye nyumba hiyo na kukutana na chanzo kimoja kilichodai kuwa baba mwenye nyumba hiyo anadai kumfumania jirani yake na mkewe kitandani.

Mke wa Bw. Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ akiondolewa eneo la tukio.
OFM YATINGA NDANI, YAKUTA MAKUBWA
OFM
ilizama ndani ya nyumba hiyo na kukuta purukushani kali ikiendelea,
Yusuf akiwa amepandwa na jazba ambapo katika kumkurupusha mgoni huyo
alijigonga mahali na kuumia usoni.
MWENYE MKE AZUNGUMZA NA OFM
Baada ya mambo kutulia, OFM ilimuuliza Yusuf nini kilitokea mpaka kuwepo kwa tukio hilo, akafunguka:
“Nilikuwa
katika harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama
anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo
jirani yangu.

“Nilipomuuliza
mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba
haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane
humu ndani.
“Ndipo
nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku
ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi.
Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa
eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga.”

MTEGO WAANDALIWA
“Kapteni
Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia mishale ya saa mbili
usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya
mawasiliano na mimi.”
JAMAA ATIA TIMU NA KIFURUSHI CHA MACHUNGWA
Yusuf
aliendelea kudai kuwa, ilipotimu saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba
Eliza alionekana akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa hatua za
kunyata na kuangalia kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi
akiwa ameshika kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na
machungwa kadhaa.

Alisema
muda mfupi baada ya kuingia, sungusungu mmoja alikwenda kujibanza
kwenye dirisha la chumba na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo
alimshuhudia Baba Eliza akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange,
sungusungu huyo akawatonya wenzake.
SUNGUSUNGU WACHOMOKA KICHAKANI
Yusuf
akazidi kusema kwamba wote walitoka kichakani na kwenda kuvamia
chumbani ambapo walimkuta mkewe aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa
sababu alijua majanga yatatokea muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya
hivyo kiaina.

JAMAA AMPIGIA MAGOTI MWENYE MKE
Baada
ya hali kuwa shwari, Kamanda wa Sungusungu, Kapteni Makumba alianza
kumsomea mashitaka jirani huyo aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na
la kusema zaidi ya kuomba radhi na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye
aliyemshawishi na haikuwa amri yake.
Ilibidi
jamaa aniombe radhi, alisema jirani yangu niko chini ya miguu yako
naomba unisamehe sitarudia tena hiki kitendo kwa kweli siyo amri yangu
ni ibilisi tu ndiye aliyeniponza, nisamehe jirani yako nakupigia magoti
unihurumie miye mkosefu,” alisema Yusuf akimkariri Baba Eliza.
...Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya kitanda iliyochafuliwa na mgoni kwa kinyesi.
APIGWA FAINI
Wakati
OFM ikiwepo eneo hilo, sungusungu walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia
Mgosi wa Ndima kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.
Mpaka
OFM inaondoka eneo la tukio saa sita na ushee usiku, Baba Eliza alikuwa
katika harakati za kumlipa fidia ya shilingi milioni moja mwenye mke.
GPL
No comments:
Post a Comment