18 June, 2014

PICHA ZINATISHA: ASKARI AUAWA KINYAMA KWA KUKATWA NA MAPANGA MKOANI PWANI...!

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi (SACP) Ulrich Mtei
Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.
Mwili wa Marehemu Muda mchache baada ya kupatwa mauti.
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH
NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi
30.
Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.

Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. 
Marehemu Joseph Ngonyani
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.

Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio hili.
AMEN

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...