18 June, 2014

VIDEO: DIAMOND AELEZEA WALICHOZUNGUMZA NA MENEJA WA TREY SONGZ, KEVIN LILES ALIPOKUTANISHWA NAYE NA RAIS KIKWETE MAREKANI


Hivi karibuni Diamond Platnumz alipata nafasi ya kukutana na mtu mkubwa
katika industry ya muziki wa Marekani Kevin Liles, ambaye ni rais wa
zamani wa Def Jam na kwasasa ni meneja wa muimbaji wa R&B Trey Songz
na Big Sean.
Platnumz ameelezea
walichozungumza alipokutanishwa na Liles na Rais Kikwete nchini
Marekani.


“Ilikuwa ni namna ya kuangalia nafanya vipi katika soko la Amerika na
dunia nzima” Alisema
Diamond. “So nilipokutana na Mheshimiwa Rais
akaniambia kitu gani unahitaji nikusaidie, nikamwambia connection, kila
kitu ni connection njia ya kuweza kuingia katika soko la Amerika na
dunia nzima, so akasema basi nitakukutanisha na mtu fulani ambaye
naamini anaweza akakusaidia, so akamtafuta akampigia simu nikaonana
naye(Kevin Liles)”.

Akizungumzia jinsi alivyo busy sasa hasa katika kujitangaza kimataifa:
“Nimekuwa nikienda speed sana kiukweli nimekuwa nikizunguka usiku na
mchana kutafuta connection…wanasema wakati unapopatikana utumie vizuri
hapo hapo unapopata sehemu hata kama kuna magoli mia piga hapo hapo
mapumziko utapumzika baadae.”
Kuhusu collabo aliyoifanya na Mafikizolo:
“Nadhani kila mtu atakuwa na rights kwa upande lets say East Afrika
nitakuwa na haki nayo mimi South Afrika wao, ikienda West ttakuwa
tunagawana labda”.
Kuhusu wimbo mpya aliomshirikisha Iyanya na video yake kufanyika na
director Mnigeria Mr Moe Musa, Diamond amesema video bado haijatoka japo
imeanza kuchezwa Channel O.
“Video kiukweli kutoka bado tho nimeambiwa kuna Channel imeanza
kupigwa (Channel O) sio mbaya lakini bado haijakuwa official released
nitawaambia”. alisema Platnumz aka Chibu!
  June 12 Diamond alitambulisha rasmi single yake mpya
‘Mdogo mdogo, ambayo hapo awali ilivuja kwa jina la ‘Kitorondo’.
 


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...