WATOTO wawili
wa familia moja, Nuru (3) na Dora Kaitaba (2), wamefariki dunia kwa
kuungua moto hadi kubaki majivu baada ya moto mkubwa uliotokana na
petroli kulipuka nyumbani kwao, Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa mashuhuda, baba mzazi wa watoto hao, Kaitaba ambaye ni mpiga picha wa kujitegemea, alikuwa amerejea kutoka Bunju B alikofuata petroli ambayo huiuza katika vipimo vidogo vya kwenye makopo ya maji nyumbani hapo.
Ilizidi kudaiwa kuwa alipofika kwake alishusha mzigo wa mafuta, watoto wake hao walikuwa wamelala katika kibanda chake cha biashara.
“Baada ya kuwasha mshumaa, moto huo ulidakwa na petroli hiyo iliyokuwa kwenye dumu na kusababisha mlipuko mkubwa.
Watu wakiwa wanaangalia tukio hilo kwa masikitiko makubwa, Kikosi cha Zimamoto Bagamoyo kiliwasili kikiwa kimechelewa hivyo kuambulia kuchukua majivu ya watoto hao wawili waliaochana mwaka mmoja kuzaliwa.
Aidha Kamanda Matei alitumia fursa hiyo kupiga marufuku biashara hiyo ya mafuta ya petroli na dizeli ambayo ni maarufu wilayani humo.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
Mtoto Dora Kaitaba (2) wakati wa uhai wake.
Tukio hilo lililowaliza wengi, lilijiri saa tatu usiku, Jumapili iliyopita watoto hao wakiwa ndani na baba yao.Kwa mujibu wa mashuhuda, baba mzazi wa watoto hao, Kaitaba ambaye ni mpiga picha wa kujitegemea, alikuwa amerejea kutoka Bunju B alikofuata petroli ambayo huiuza katika vipimo vidogo vya kwenye makopo ya maji nyumbani hapo.
Ilizidi kudaiwa kuwa alipofika kwake alishusha mzigo wa mafuta, watoto wake hao walikuwa wamelala katika kibanda chake cha biashara.
Mtoto Nuru Kaitaba (3) enzi za uhai wake.
Ghafla,
mashuhuda wanasema, umeme ulikatika hali iliyomfanya Kaitaba kuchukua
mshumaa na kuuwasha ili andelee na shughuli zake za kuhudumia wateja.“Baada ya kuwasha mshumaa, moto huo ulidakwa na petroli hiyo iliyokuwa kwenye dumu na kusababisha mlipuko mkubwa.
Mama mzazi wa wa watoto hao (aliyenyosha mikono) akiwa na simanzi kwa kuwapoteza wanaye.
Mashuhuda
walisema Kaitaba alikimbia kutoka bandani, lakini alipopata akili ya
kuwaokoa watoto wake tayari moto ulishakuwa mkubwa na hivyo kumfanya
apige kelele za kuomba msaada.
Mchungaji akiziombea roho za marehemu hao, zikapate kupumzika kwa amani.
Hata hivyo, majirani walishindwa kuingia ndani kutokana na ukubwa wa moto huo na uduni wa vifaa vya kuzimia.Watu wakiwa wanaangalia tukio hilo kwa masikitiko makubwa, Kikosi cha Zimamoto Bagamoyo kiliwasili kikiwa kimechelewa hivyo kuambulia kuchukua majivu ya watoto hao wawili waliaochana mwaka mmoja kuzaliwa.
...Ndugu na jamaa wa karibu wakiwaaga watoto hao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Onesphory Matei amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema tofauti na madai ya baadhi ya watu kuwa baba
mzazi wa watoto hao anashikiliwa na polisi, alichukuliwa na kupelekwa
hospitali kwa ajili ya kutibiwa majeraha na hatachukuliwa hatua yoyote
kwa vile kilichotokea ni ajali.Aidha Kamanda Matei alitumia fursa hiyo kupiga marufuku biashara hiyo ya mafuta ya petroli na dizeli ambayo ni maarufu wilayani humo.
Wakinamama wakipanda gari kuelekea kwenye mazishi ya watoto Nuru na Dora.
Marehemu walizikwa Jumatatu iliyopita kwenye Makaburi ya Bunju, Kinondoni, Dar.Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment