Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana walitoa ufafanuzi wa hoja
mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika mjadala uliofanyika hapa
kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu kumshangilia, bali
walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na wakilifuata na
kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe wenzake, Profesa Palamagamba Kabudi,
Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu Malale na Awadh Ali Said
walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba lililoandaliwa na Taasisi
ya Mwalimu Nyerere jana.
Jaji Warioba ndiye alianza kuzungumza kwa kukanusha madai
yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa amepeleka maoni mapya
serikalini.
Alisema madai hayo hayana ukweli bali maoni aliyowasilisha
serikalini yalitokana na maoni ya wananchi waliyokusanya wakati
wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza kusaidia katika
kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Juzi, katika mdahalo uliorushwa na Star TV, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alidai
kuwa Jaji Warioba amewasilisha serikalini maoni mapya, ukiacha yale
ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Jaji Warioba alisema Tume iliandaa sura ya kwanza iliyohusu
mali na maliasili na sura ya tano kuhusu Serikali ya Muungano na sura ya
nne iliyoelezea serikali za mitaa.
“Sura ya nne na tano tulibaki nazo lakini Machi 27, mwaka huu
niliandika barua kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na Chikawe (Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe) kwa kuwa
alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria kipindi hicho na nikawakabidhi ili
isaidie katika mchakato wa Katiba hasa wakati wa kuandaa Katiba ya
Tanganyika,” alisema Jaji Warioba.
Aliongeza; “Hayakuwa mawazo mapya wala sikupeleka mawazo
mapya, bali ni mawazo tuliyoyakusanya kutoka kwa wananchi na nimeamua
kufanya hivyo kwa kuwa tume kwa kipindi chote ilikuwa wazi na mimi
nimeamua iwe ‘public’ (wazi) kwa kila mmoja kujua, ili iwasaidie kujua
wakati wa uandaaji wa Katiba ya Tanganyika.”
Jaji Warioba pia alifafanua sababu za tume kupendekeza muundo
wa serikali tatu, kwamba haikufanya hivyo kutokana na idadi ya watu
waliotaka muundo huo, bali ilitizama uzito wa hoja zilizotolewa.
“Wapo wanaosema kuwa idadi ya watu waliotaka muundo wa
serikali tatu ni wachache. Tulipendekeza muundo huo kwa sababu ya hoja
zilizotolewa na siyo wingi au uchache wa waliotoa maoni,” alisema.
Alisema hoja ya kwanza ni Tanganyika kuvaa koti la Muungano
pia akifafanua jinsi Tanzania Bara inavyoshughulikia masuala yake ya
kiuchumi bila kugusa masuala hayo kwa upande wa Zanzibar.
“Leo hii mawaziri wangapi wa muungano wanaotembelea Zanzibar
kukagua shughuli za maendeleo, pia kuna mgongano wa Katiba ya Tanzania
Bara na Zanzibar. Pia suala la fedha nalo limekuwa na mvutano kwa muda
mrefu hasa kuhusu pande hizi mbili kuwa na akaunti ya pamoja,” alisema
na kuongeza:
“Wajumbe wa tume tulikuwa na itikadi tofauti lakini hata siku
moja hatukuwahi kupiga kura kupitisha jambo lolote, kila
tulichokipendekeza tulikubaliana. Nadhani waendelee na majadiliano ili
wafikie mwafaka,” alisema.
Alisema hata kama mchakato wa Katiba utasitishwa kwa muda,
jambo la msingi linalotakiwa kuheshimiwa ni kuachwa kwa maoni ya
wananchi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba.
Butiku: JK alitetea masilahi ya CCM
Katika mchango wake, Butiku ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, alisema hotuba ya Rais Jakaya Kikwete
wakati akilifungua Bunge Maalumu la Katiba ililenga kutetea masilahi ya
CCM.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria, Butiku
alisema CCM imeficha maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume kwa muda
wa miezi 18, vikiwamo vitabu mbalimbali vya mapendekezo ya Watanzania
kuhusu nini wanataka kiwemo katika Katiba yao.
Hata hivyo, katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi aliyoitoa
Alhamisi iliyoipita, Rais Kikwete alijivua lawama kuwa ndiye alikuwa
chanzo cha kuvurugika kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Butiku alianza kwa kuuliza, “Nani anaficha maoni” watu
wakaitikia “CCM”, akauliza tena, “Huyu anayeficha maoni anatuheshimu
hatuheshimu,” wasikilizaji wakaitikia, “Hatuheshimu.”
Akijibu kauli ya Rais Kikwete wakati akilifungua Bunge la
Katiba, Butiku alisema: “Unaposema ukweli hutakiwi kuuminya. Rais
Kikwete alisema mashauriano kati yake na wajumbe wa tume hayakuwa ya
kina, lakini ukweli ni kwamba mashauriano yetu yalikuwa ya kina.”
Aliongeza: “Tunaheshimu maoni yake aliyoyatoa ila kuna maoni
aliyotoa yalioonekana kuelekea kuitetea CCM na kama mnakumbuka katika
hotuba yake alikuwa akisisitiza kwamba ‘Tumieni akili zenu mjadiliane na
kupata uamuzi.”
Huku akinukuu baadhi ya vifungu vya Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba vinavyoeleza jukumu la Bunge Maalumu la Katiba, Butiku alisema
kilichoandikwa katika Rasimu ya Katiba ni maoni ya wananchi na ndiyo
yanayotakiwa kuheshimiwa kama inavyoeleza sheria hiyo.
“Huu haukuwa mchakato wa kienyeji, nasema wazi mimi ni
mwanachama wa CCM lakini sitarajii Rais awe na kikundi cha kwenda
kuuliza kuhusu utekelezaji wa masuala ya kitaifa. Katika hili CCM
tumekosea,” alisema Butiku.
Aliongeza: “Tume ilitoa vitabu na takwimu mbalimbali ambazo
ziliwekwa katika tovuti ambayo imefungwa. Kuna nyaraka mbalimbali ambazo
Tume ilizikusanya baada ya kukusanya maoni lakini zimefichwa.”
Akizungumza kwa njia ya kuuliza zaidi maswali, Butiku alisema
kama muundo wa serikali tatu umekuwa na mgogoro je, ni sawa kuwa na
muundo wa serikali mbili wenye nchi mbili?
Alisema hakuna aliyekataa muundo wa serikali mbili, ila
muundo huo unatakiwa kufanyiwa maboresho makubwa ambayo utekelezaji wake
ndiyo tatizo… “Inakuwaje leo watu wazima tunabishana jambo lililo wazi
kabisa wakati suluhisho tunalijua?”
Polepole na gharama za serikali tatu
Polepole ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi za Kiraia alisema
kauli ambazo zinatolewa kuhusu gharama za kuendesha serikali tatu hazina
ukweli wowote kwani katika rasimu hiyo wamebainisha vyanzo vya mapato.
Polepole alisema waliiandikia barua Hazina kuomba taarifa
zitakazotumika kuendesha Serikali ya Muungano na kwa mwaka 2011/12
bajeti ilikuwa Sh1.4 trilioni, mwaka 2012/13 (Sh1.8 trilioni) na mwaka
2013/14 ni Sh1.9 trilioni.
“Kwa kiwango hiki, Serikali ya Muungano haitakuwa na gharama
zozote zile za ziada na kinachojitokeza sasa ni tatizo la masilahi
binafsi,” alisema Polepole na kuongeza: “Watu wanataka serikali mbili
kwa sababu ina mambo yote ya Muungano na Tanganyika kwa sababu ndiyo
inayoteua wakurugenzi, makatibu wakuu na wengineo, hivyo wakipata urais
wanalipana fadhila.”
Alisema wakati wakikusanya maoni, makatibu wakuu wa Serikali
ya Zanzibar walipendekeza serikali tatu, kamati ya makatibu wakuu
Serikali ya Muungano walipendekeza serikali mbili lakini zilizoongezwa
mambo ya Muungano.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia mambo yote ya
Tanzania bara ilipendekeza serikali tatu na Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano iliyopewa dhamana ya kuimarisha Muungano ilipendekeza serikali
tatu.
“Kwa hali yoyote ile huwezi kuepuka mapendekezo yaliyomo
katika Rasimu kwani yataondoa kero zilizopo kwa pande zote,” alisema
Polepole.
Kabudi atoa somo
Akitoa mchango wake, Profesa Kabudi alisema: “Nchi hii ni
kubwa kuliko sisi sote, hakuna mkubwa zaidi ya nchi hii, sisi sote
tutakufa, tutazikwa na tutaoza lakini nchi hii itaendelea kuwapo.”
Alisema kuhusu Muungano, Wazanzibari wanazungumza kuliko
Watanganyika, lakini ukifika wakati Watanganyika wakazungumza, itakuwa
hatari hivyo akasema ufike wakati Watanganyika wapewe serikali yao
wakati wakiogopa, wasisubiri waanze kuidai Tanganyika yao.
Alisema baada ya kuvurugwa kwa Kongo, Tanzania ndiyo imekuwa
kama nyonga ya Afrika na kuwa na umuhimu wa kipekee kwa ulinzi wa nchi
nane zilizoizunguka na Bahari ya Hindi.
Alishangazwa na hatua ya kuwekwa kando kwa tume baada tu ya
kuwasilisha Rasimu ya Katiba na kwamba hatua hiyo ndiyo chanzo cha
mkwamo uliopo kwa sasa kwa kuwa ndiyo iliyokuwa ikijua chanzo na kila
ibara na sababu za kuwapo kwake, hivyo ingeweza kutoa ufafanuzi pale
ambako litatokea tatizo.
Wakati akitoa kauli hiyo, watu waliofurika katika ukumbi huo
walilipuka kwa shangwe, “Sema usiogope sema,” huku Profesa huyo
akihitimisha kwa kuwataka Watanzania kujadili mambo hayo kwa ajili ya
mustakabali wa Taifa.
Awadh azungumzia misukosuko
Awadh ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) alisema Muungano umefika hapa baada ya kupitia misukosuko mingi.
“Hakuna sehemu Tume iliambiwa itumie takwimu, bali ni hoja
zinazofanana na kutofautiana na kufanya uamuzi, ndicho ambacho tulikuwa
tukikifanya wakati wote,” alisema na kuongeza: “Watu wengi suala la
muungano hawalielewi na wanaupotosha umma. Muungano unatakiwa kuweka
haki sawa, fursa sawa na hadhi sawa, lakini usipokuwa na haya hatuwezi
kuwa na muungano imara.”
Alitoa angalizo kwa wanasiasa kuzungumza kama wachumi hasa
katika gharama, jambo ambalo hawana uzoefu na uelewa nalo akisema
wanaongeza vitu visivyo na ukweli ndani yake.
Malale: Hatuwezi kutumia maoni kama kichaka
Malale alisema kuwa Tume ilikusanya maoni ya wananchi nchi
nzima na kamwe haiwezi kuyatumia kama kichaka, kama wanavyofanya watu
wengine.
“Watu waache kutumia maoni ya wananchi kama kichaka cha hoja
zao. Tume imechukua maoni ya wananchi na kuyaweka kwa pamoja. Maoni yao
yanatakiwa kuheshimiwa na yasitumike kama kichaka kwa wengine,” alisema
Malale.
Jaji Warioba alihitimisha mdahalo huo kwa kuwajibu wanasiasa
wanaodai kuwa takwimu za idadi ya wananchi waliotoa maoni si sahihi
kutokana na idadi kupishana kati ya Mkoa wa Kigoma na Tabora.
“Kwani wananchi wa Kigoma siyo Watanzania? Jumla ya wananchi
8,600 walitoa maoni mkoani Kigoma na wananchi 3,011 mkoani Tabora,”
alisema na kuongeza: “Mkoa wa Kigoma na Kagera ndiyo iliyoko pembezoni,
hivyo ina matatizo lukuki ndiyo maana walijitokeza kutoa maoni kwa wingi
ili yaingizwe katika Katiba.”
Alisisitiza kuwa hata kama yatazungumzwa maneno gani, Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ndiyo iliyohoji wananchi, hivyo inajua kila jambo
walilopendekeza na kipi ambacho wananchi wanakitaka.
Alipoulizwa nini hatma ya Bunge Maalumu la Katiba kutokana na
baadhi ya wajumbe wake kususia vikao vyake alisema: “Nawashauri waache
masilahi binafsi ya makundi yao na wafanye kazi. Wajifiche chumbani na
wapate mwafaka wa kuijadili rasimu.
Fidelis Butahe na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana walitoa
ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika mjadala
uliofanyika hapa kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu kumshangilia,
bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na wakilifuata na

MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment