IBARA 28 ZA TUME YA WARIOBA ZILIZOONDOLEWA
RASIMU ya Katiba inayopendekezwa iliyowasilishwa bungeni juzi, imeondoa Ibara 28 zikiwamo zinazowataka viongozi wa umma kutopokea zawadi kwa manufaa yao binafsi wala kufungua akaunti ya benki nje ya nchi pasipo sababu maalumu, Mwananchi limebaini.
Ibara ya 15 iliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ilisema: “Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ilitaka Bunge kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano. Mbali na ibara hiyo, pia Ibara ya 16 iliyohusu ufunguaji akaunti nje ya nchi, imeondolewa.
Ibara nyingine zilizoondolewa ni pamoja na ya 17 iliyopendekeza uwazi wa mali ikimtaka kiongozi wa umma kutangaza thamani ya mali na madeni yake mara tu baada ya kupata uongozi.
Pia Ibara ya 129 iliyokuwa inawaruhusu wananchi kumvua madaraka mbunge ambaye atashindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake au ataacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la jimbo la uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi imeondolewa.
Ibara 28 zilizoondolewa
15. (1) Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa katibu mkuu wa wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:
(a) aina ya zawadi; (b) thamani ya zawadi; (c) sababu ya kupewa zawadi; na (d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.
(2) Neno “zawadi” kama lilivyotumika katika ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani atakachopewa kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.
(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.
129. - (1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, wananchi watakuwa na haki ya kumwondoa mbunge wao madarakani, endapo mbunge atafanya moja wapo au zaidi ya mambo yafuatayo:
(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na masilahi ya wapigakura au kinyume na masilahi ya Taifa;
(b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi; au
(d) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya nchi.
(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya kuendesha uchunguzi kwa Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapigakura wake na utaratibu wa kumwondoa katika ubunge.
146.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kusema uongo bungeni na kwa sababu hiyo, mbunge anapozungumza ndani ya Bunge ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha.
(2) Mbunge anapokuwa akizungumza bungeni hatahesabika wala kutafsiriwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo lililotangazwa au lililoandikwa na vyombo vya habari au nyaraka nyingine yoyote ambayo chanzo chake kinafahamika au kitaelezwa na mbunge huyo.
©Mwananchi, 2014.

No comments:
Post a Comment