Msemaji
wa Jeshi la Polisi, Advera Senso akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani), Septemba 3,2014 kuhusu kupiga marufuku watu wanaotumia
mitandao kinyume na taratibu.
Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo kwa
watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi,
uchochezi, picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa Serikali,
dini na watu mashuhuri.
Akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3,2014
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa tayari baadhi ya watu
wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na wengine
wanaendelea kuhojiwa.
"Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu
kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kinyume na malengo
yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi, kashfa,kuchafua
viongozi wa Serikali."Wengine wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo
hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina, ingawaje mwingine anaweza
hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.
Senso aliendelea kubainisha kuwa kuvunja
kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu ya kuepuka kuchukuliwa hatua
za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila kujali anaifahamu
sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.Alisema oparesheni ya kuwabaini
wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina
hiyo.
Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inawatia
hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya utapeli na kujipatia
kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs zinazosambaza picha
chafu ambazo ni kinyume na maadili."
Wapo baadhi ya watu wanatumia mitandao ya
simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu ya waharifu
wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa hatua kali
zitachukuliwa dhidi yake," alisema.
Hivyo alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa
onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu huo, na kuwataka wale
wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali waufute.
No comments:
Post a Comment