Msanii mkongwe wa filamu nchini, Blandina
Chagula maarufu
kama Johari, ambaye ni ‘business partner’ wa msanii mwenzake, Vicent
Kigosi aka Ray, amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na Ray pamoja
na mipango yake ya kuolewa. Akizungumza na na chanzo makini cha
kuaminika leo, Johari amesema anashangazwa kuwaona watu wakivumisha kuwa
na mahusiano ya kimapenzi na Ray.
“Mimi na Ray cha kwanza ni mtu na swahiba wake, cha pili
ni kama kaka yangu kwasababu tumekaa kwa muda mrefu sana. Tumefanya kazi
kama partner wangu, tuna ukaribu ambao upo kikazi zaidi na kampuni
yetu, lakini uhusiano mwingine ambao watu wanauzungumzia sidhani kama
upo ni maneno ya watu,” amesema. “Hatujawahi kutokea uhusiano wa
kimapenzi na Ray. Unajua kuna watu wanaongea vitu vya kubuni, mimi na
Ray tunafanya kazi kampuni moja na wote ni wakurugenzi kwahiyo inamaana
tungekuwa tuna ugomvi tungevunja kampuni. kama hicho hakipo na bado tunafanya kazi
vizuri na tunaheshimiana na kila mmoja kampuni inampatia maisha mazuri.
Kwa sasa sijaolewa lakini siwezi kuweka wazi sana mahusiano yangu kwa
sababu muda haujafika ila muda utakapofika Nitawaweka wazi.
No comments:
Post a Comment