Kamishna wa kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA akiwasili katika viwanja vya polisi Osterbay tayari kabisa kuhudhuria sherehe hizo za ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani. |
Wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa kanda ya Dar es salaam imezinduliwa jana tarehe 22 na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Jordan Rugimbana katika
sherehe zilizofanyika katika makao makuu ya polisi Wilaya ya Kinondoni Ostabay jijini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo kamishna
wa kanda maalum ya Dar es Salaam SULEMAN KOVA na makamanda wengine wengi
pamoja na wananchi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam.
Akizungumza
wakati akisoma risala iliyokuwa isomwe na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. SAID MECK SADIC Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Jordan Rugimbana amewatahadharisha
madereva na watumiaji wa barabara kuwa makini pindi wawapo barabarani
ili kuepusha ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikijitokeza
kutokana na uzembe wa madereva na watuamiaji wa barabara kwa ujumla.
wiki ya nende kwa usalama baranbarani kitaifa ulifanyika Mkoani Arusha
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA SHEREHE HIYO YA UFUNGUZI
Kamishna Kova akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Kinondoni wakati wa shughuli hiyo. |
Wanafunzi ni sehemu ya wageni waliofika hapa ili kupata elimu ya usalama barabarani |
Kikundi cha sanaa ambacho kilikuwa kikitoa burudani wakati wa uufunguzi huo |
Maandamano kuingia uwanjani hapo yalifanyika kutoa jumbe mbalimbali kuhusu wiki hii |
Kamishna wa kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA akitoa elimu ya usalama barabarani mbele ya watu waliohudhuria katika sherehe hizo fupi. |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Jordan Rugimbana akisoma hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye alitoa hudhuru mkuu wa mkoa wa Dar es salaam SAID MECK SADIC |
Picha ya pamoja |
Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni akikata utepe kuashiria kuwa wiki ya nenda kwa usalama barabarani imezinduliwa rasmi katika kanda ya Dar es salaam ambapo kitaifa imefanyika Arusha |
Mgeni rasmi akipata maelekezo mbalimbali kutoka katika mabanda yanayotoa elimu ya usalama barabarani katika viwanja hivyo |
No comments:
Post a Comment