Kivuko cha MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya Kusini.
Kivuko hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi za kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga barabara za New Bagamoyo (Kawawa JCT – Tegeta); ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit Infrastructure – BRT) ikiwemo kuanza ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili ; ujenzi wa ‘Flyover’ ya TAZARA na UBUNGO ; barabara za pete (DSM Outer Ring Roads); barabara ya Dar es Salaam – Chalinze Expressway; kupanua barabara ya lami sehemu ya Gerezani (KAMATA – Bendera Tatu) kutoka njia mbili za sasa hadi njia nne; kujenga daraja la Kigamboni linalounganisha Kurasini na Kigamboni, daraja hili linatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa sita.
Ads by Cinema-Plus-1.5cAd Options
No comments:
Post a Comment