Wachunguzi wa Kijerumani dhidi ya ndege ya
abiria ya Malaysia ambayo ilipata ajali huko Ukraine mwezi July na
kuripuka angani wanaeleza kua ndege hiyo baada ya kukumbwa na kitu
chenye ncha na kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali ndio
chanzo cha ajali.
Mwandishi wa BBC amesema kwamba ushahidi huo ni wawazi na kwamba
ndege hiyo ilishambuliwa kwa kombora..katika ripoti yao ya kwanza ya
kiuchunguzi ,maafisi wa kijerumani katika masuala ya usalama wa anga
wameeleza kua hakukuwa na tatizo la kiufundi lililosababisha ndege hiyo
ipate ajali, ama makosa ya rubani yalosababisha ndege aina ya MH17
kuripuka.Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba kisanduku cha kurikodia mwenendo wa ndege hiyo hakikuonesha kwamba kulikua na dharura.
Abiria wote miambili na tisini na nane walipoteza uhai pindi ilipo anza safari kutoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kueleke Kuala Lumpur.kutokana na ajali hiyo kuna shaka kwamba vikundi vya waasi wa Urusi viliiidungua ndege hiyo.Lakini mpaka sasa Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na ajali hiyo.
Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege hiyo MH17 inaweza kupatikana pindi mwakani.
Ads by Cinema-Plus-1.5cAd Options
No comments:
Post a Comment