MUUNGANO wa Tanzania ni muungano wa damu na wa watu,
ambapo Ibara ya kwanza Sura ya kwanza inaeleza kuwa msingi mkuu wa Jamhuri ya
Muungano pamoja na katiba iliyopo na inayopendekezwa ni haki ya makubaliaono ya
mwaka 1964.
Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Mary Nagu wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge
hilo kuhusu mambo mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.
Mhe. Nagu amesema kuwa Hati ya Makubaliano hayo
imejengeka katika misingi ya utu, udugu na kuaminiana ambapo Waasisi wa
muungano huo hawakupeleka maslahi yao wenyewe binafsi wala kuzingatia suala la
mali, bali walizingatia umuhimu na mahitaji
ya muungano kutokana na mambo hayo makuu matatu.
Ameeleza kuwa mambo wanayoyajadili bungeni hapo kwa
sasa ndiyo yatatokana na muungano ambao una mfumo bora na muundo bora.Mhe. Nagu amebainisha kuwa wale viongozi wenye kutaka
muungano wenye gharama kubwa watawafanya wengine washindwe hapo baadaye.
“Naomba sana tuendelee na kuona kuwa muungano huu ni
muhimu nataka niwaambie kwamba Zanzibar ni lango kuu la Jamhuri ya muungano wa
Tanzania na lango hili linatuhakikishia usalama wetu na ulinzi wetu kwahivyo na
Wazanzibar nao wanufaike na rasilimali za Bara, kwahiyo muungano huu ni muhimu
na utanufaisha pande zote mbili mimi sina wasi wasi”, alisema Mhe. Nagu.
Aidha, Mhe. Nagu amegusia suala la usawa wa jinsia
kupitia hamsini kwa hamsini katika uwakilishi, ajira na maeneo mengine.Mhe. Nagu ameleza kuwa usawa wa jinsia utajenga jamii
nzuri ya Tanzania ikiwemo kuleta heshima pamoja na haki katika jamii hiyo kwani
kwa mila na desturi za Waafrika na Watanzania, wanaume hawakupaswa kuwa
wamiliki wa kila kitu.
“Akina baba ni Custodians lakini wakajigeuza wamiliki, tunachotaka waendelee
kuwa Custodians na sisi watuone ni wenzao, kwahivyo suala la jinsia halina
mjadala, kupitia uwakilishi teundelee na hamsini kwa hamsini na Katiba iseme
wazi, mengine yatajitokeza kwenye Sheria ya uchaguzi”. Alisisitiza Mhe. Nagu.
Kuhusiana na suala la ajira na uongozi Mhe. Nagu ameeleza
kuwa wanawake zaidi ya asilimia 52% wangepaswa kuwa katika kila eneo lakini
hawapo na suala hilo linaleta tofauti isipokuwa mashambani ambapo chakula chote
kinachotoka kwa kiasi kikubwa wanaolima ni wanawake.

No comments:
Post a Comment