Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
17 September, 2014
MWANAMKE AJIRUSHA KWENYE BWAWA LA MAMBA
Mwanamke
mwenye umri wa miaka 65 mjini Bangkok, Thailand, amefariki baada ya
kujirusha katika bwawa lenye Mamba katika shamba la kutunza na kuhifadhi
wanyama hao karibu na mji huo.
Walioshuhudia kitendo hicho
wanasema kuwa walimuona mwanamke huyo, Wanpen Inyai, akijirusha katika
bwawa lenye Mamba katika kituo cha kuwatunza wanyama hao cha Samut
Prakarn, siku ya Ijumaa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la The Bangkok Post. Wafanyakazi wa kituo hicho walikosa kumuokoa mama huyo.
Polisi
wanasema kuwa walifahamishwa na familia ya mama huyo kwamba alionekana
mwenye afya duni na mwenye kusongwa na mawazo kabla ya kifo chake.
Kituo hicho kina zaidi ya Mamba 100,000 katika mabwawa yake
Vituo vya watalii nchini humo vinasemekana kukosa mikakati ya usalama.
Polisi walithibitisha kifo cha Bi Wanpen Jumanne mchana.
Kwa
mujibu wa ripoti, Bi Wanpen alivua viatu vyake kabla ya kujirusha ndani
ya bwawa hilo, ambalo linasemekana kuwa na kina cha mita tatu.
Wafanyakazi walijaribu kutumia vijiti virefu kuwafukuza Mamba hao kwa lengo la kuwazuia wanyama hao kumshambulia mwanamke huyo.
Mapema
siku hiyo, familia ya Wanpen, ilijaribu kutoa taarifa ya kupotea kwake
la lengo la kumtafuta ingawa walifahamishwa kusubiri kwa saa 24.
Kifo
chake kinafanana na kisa kimoja kilichomkumba mwanamke aliyejiua mwaka
2002 kwa njia hiyo hiyo katika kituo cha kuwatunza Mamba.
No comments:
Post a Comment