09 September, 2014

SAMWEL SITTA KWA UNAFIKI WAKO HUU,UNASIFA YA KUJIITA WEWE MZALENDO?SOMA HAPA KUJUA

Na Edson Kamukara
    KAMA ni hadaa za kisiasa kwa Samuel Sitta, basi tuna kila sababu ya kumshauri kwamba imetosha, maana lengo lake la kujijenga kisiasa linazidi kuyeyuka na sasa ni kama anajitengenezea fedheha ya historia.
           Sitta alivuma sana wakati alipochaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tisa, pale alipoingia kwa falsafa ya Kasi na Viwango, akijitutumua kwamba anapambana na ufisadi lakini mwishowe ilibainika kuwa alikuwa analipa visasi kwa wenzake wa kundi la mtandao ndani ya CCM baada ya kuukosa uwaziri mkuu.
            Mwaka huu, Sitta alichaguliwa na wajumbe wenzake wa Bunge Maalum la Katiba kuwa mwenyekiti wa Bunge hilo. Falsafa aliyoitumia ni kwamba kumweka yeye kwenye kiti hicho ni sawa na kumpiga teke chura kumrejesha majini alikozoea.

               Tambo zote sasa zimeyeyuka na Bunge la Katiba limekwama lakini Sitta bado anajaribu kujihalalisha kwa sifa ambazo kimsingi hana tena.
           Sitta anajiita mzalendo anayefanya kazi ya kizalendo ya kuwaletea Watanzania Katiba mpya halafu anasimamia kuvunja wa sheria ya mabadiliko ya katiba inayoeleza bayana majukumu ya Bunge Maalum.
         Kwa faida ya wasiofahamu, neno uzalendo kwa mujibu wa Kamusi ya Kiwahili Sanifu ni hali ya mtu kuwa tayari kuifia nchi yake. Je, ni kweli Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, matendo yake ni ya kuifia nchi yake au chama chake nayeye binafsi? Tujadiliane tuone.
            Wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na washirika wao kutoka vyama mbalimbali vidogo vya siasa na makundi ya kundi la wajumbe 201 wa kuteuliwa na Rais wako mjini Dodoma, wakiendelea na mjadala wa rasimu ya Katiba bila wenzao wa kundi la UKAWA.
        Sababu ya kutokuwepo kwa wajumbe wa UKAWA inajulikana wazi kwamba ni baada ya kuona CCM wanatumia wingi wao kupindua rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo kimsingi ndiyo imebeba maoni ya wananchi na kumbe jukumu la Bunge la Katiba ilikuwa ni kuyaboresha.
            Jitihada za UKAWA kurejea bungeni zimegonga mwamba baada ya vikao vya maridhiano mbali mbali kukwama, kikiwemo pia alichokiitisha Sitta mwenyewe jijini Dar es Salaam na hivyo kuufanya mchakato huo kukwama kutokana na theluthi mbili ya kura za uamuzi kutopatikana hususani Zanzibar.
           Pamoja na ugumu huo, bado Sitta kwa kushirikiana na chama chake walilazimisha Bunge liendelee na vikao huku wakifahamu fika mwisho wa siku hawawezi kufanya uamuzi wa kura.
             Kelele zimepigwa kila kona za kutaka mchakato huo usimame kwanza hadi maridhiano yapatikane kwa sababu katiba inayotafutwa sio ya CCM wala UKAWA, lakini Sitta anajibu kwamba yeye na wenzake ni wazalendo na kwamba UKAWA si wazalendo.
             Hapa ndipo naanza kuhoji uzalendo wa Sitta ni upi? Anamaanisha kitendo cha wajumbe kula posho ya sh. 300,000 halafu mwisho wa siku hawataweza kufanya uamuzi wa kupitisha katiba inayopendekezwa kwenda kwa wananchi?
          Je, uzalendo wake ni wa kuhadaa makundi mbalimbali kwenda kukutana naye mjini Dodoma na kumpelekea maoni yao ili yaingizwe kwenye mjadala wa rasimu wakati kazi hiyo ilikwishamalizwa na Tume ya Jaji Warioba?
            Hivi kweli hata kama CCM wameishiwa na aibu, Sitta bado anakubali kuendelea kujidhalilisha kiwango hiki halafu anathubutu kujiita mzalendo wakati anasimamia uvunjaji wa sheria?
           Kama ndani ya CCM kwenyewe wanakong’ang’ania muundo wa serikali mbili kiasi cha kufumua rasimu na kuigeuza bila kuamua muundo wa muungano, wameshtuka kwamba katiba mpya haiwezekani bila maridhiano na sasa wanapingana wazawazi, huo uzalendo wa Sitta ni upi?
          Tuamini uzalendo wa Sitta upo kwenye kuendesha Bunge la katiba kwa hisia kwamba wao CCM wajadili tu ila mwisho ana uhakika wajumbe wa UKAWA watarudi kupiga kura?
          Kama Sitta anao uhakika huo wa kupatikana kwa kura theluthi mbili ya kupitisha katiba inayopendekezwa, kwanini hakutumia uzalendo anaojivika kumwondoa hofu Mwanasheria Mkuu wa Sreikali, Jaji Fredrick Werema.
          Wiki mbili zilizopita, Jaji Werema aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, akasema kuwa kwa jinsi mchakato unavyokwenda, kuna hofu ya theluthi mbili kutopatikana na kwamba serikali inaangalia utaratibu wa kurudi kwenye Bunge la Jamhuri kufanya mabadiliko ya 15 ya katiba katika baadhi ya vipengele muhimu.
        Kwa mujibu wa Jaji Werema, vipengele hivyo ni kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi, kuruhusu uwepo wa mgombea binafsi na kupunguza madaraka ya Rais.
       Nimeomba wewe msomaji wa fikra mpya tujadili kwa pamoja huo uzalendo wa Sitta ambaye anashindwa hata anapingana na serikali anayoitumikia, maana kama Jaji Werema ana hofu ya katiba mpya kutopatikana, Sitta anaishi dunia gani?.
        Lakini yafaa tukumbuke kwamba Sitta hajaanza usanii wake katika Bunge la Katiba, la hasha! Huyu kipindi akiwa Spika wa Bunge la Tisa, alitumia sh. zaidi ya milioni 100 kuchunguza tuhuma za mbunge wa Mkuranga, Adam Malima dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
         Lakini cha kushangaza kiongozi huyo, aliyejitapa ni mpambanaji wa ufisadi hakuchukua hatua yoyote ya kinidhamu dhidi ya Malima licha ya kuthibitika alilidanganya Bunge.
        Mzalendo huyo anayewanyooshea wenzake vidole akisema wamechafuka kwa ufisadi hawafai kupewa nafasi ya kugombea urais ndani ya CCM, alitumia mabilioni mengine katika Kamati Teule ya Bunge kuchunguza zabuni tata ya kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond, lakini baada ya mbaya wake kisiasa aliyemlenga, Edward Lowassa, kujiuzulu uwaziri mkuu, alifunga mjadala wa sakata hilo kibabe bungeni.
           Ni Sitta huyo huyo mzalendo asiyeona aibu ya wajumbe kulipwa posho wakati wanajadili jambo tofauti na kazi waliyokabidhiwa, aliamua kutumia mabioni ya umma kujenga ofisi ya Spika nyumbani kwake Urambo Mashariki.
        Ofisi hiyo sasa haiwezi kutumiwa hata na Spika wa sasa Anne Makinda kwa sababu hawezi kufanyia shughuli za Bunge akiwa Urambo Mashariki. Katika machache haya ni nani anaweza kudanganywa kwamba Sitta ni mzalendo (mtu wa kuifia nchi yake) na akamkubalia? Tafakari

Kwahili Mhe Samweil SITTA umezidi hata kama unamatatizo ya AKILI basi wahusika wakufunge KAMBA au wakupeleke MILEMBE.
Mwenyekiti wa BUNGE Maalumu la KATIBA jana alitoa dakika 10 kwa mjumbe wa BUNGE hilo "Kujibu Mapigo" dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Self Sharrif Hamad kinyume na kanuni za BUNGE hilo.
Sitta akimkaribisha Hamad Rashid Mohamed alisema anatumia Kanuni ya 27(1) (e) ya BINGE hilo ambayo inampa mamlaka ya kuingiza shughuli yoyote anayoiona inafaa na kwa jana shughuli aliyoiona inafaa ni kumpa Hamad Rashid nafasi kujibu mapigo kwa kumshambulia kiongozi wa nchi ya Zanzibar.
Mwanasheria msomi na Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar-es Salaam James Jesse amesema "Hatua hiyo si sahihi, hatuna sheria inayotoa haki ya kujibu mapigo bungeni kama ilivyo kwa nchi za wenzetu ambapo mtu akishambuliwa bungeni anapewa haki ya kwenda kujibu na majibu yake yanaingia katika hansard (kumbukumbu za bunge) Pamoja na kwamba kanuni inasema inatoa mamlaka hayo kwa mwenyekiti, kitu chochote lazima kiwe na mipaka.
"Kwa kuwa kitu kinachojadiliwa ni KATIBA na si kingine, hiyo nafasi ya kuzungumza mambo mengine haikuwepo"
NB Ikumbukwe kuwa Mhe SITTA anajiona ni MJANJA sana wa kucheza na AKILI za watu. serikali 3 ni lazima
‪#‎UKAWA‬

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...