Naomba kuwasaidia BAVICHA, ni kwa dhati ya moyo wangu
“...wakristo wanajuakuwa Mussa alianzisha safari ya waisrael kwenda
Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (edwin), Kimesera (Victor), Bob
Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila
hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu..”
Maneno hayo kwenye aya niliyoinukuu hapo juu si yangu bali ni ya
EmmanuelMasonga Mwenyekiti wa BAVICHA kutoka wilaya ya njombe akimsifu
Mbowe mbele ya Wazee wanaojiita “..wazee wa CHADEMA..” jijini Dar
essalaam.
Labda niseme ni kujitia Upofu, labda niseme Mapenzi
yaliyopitiliza na wakati mwingine napata dhana kuwa ni UMBUMBUMBU, na si
kingine chochote kinachowafanya Vijana wa BAVICHA
kutojitathimini,kutojiuliza na kutofikiri sawasawa kabla ya kutoa kauli,
hasa kauli hiyo ikitolewa kwenye kongamano la watu.
Yapo mambo sisi
vijana tukiyafanya, yanatudhalilisha, yanatufedhehesha mbele za watu na
mbaya zaidi yanatushusha hadhi na kututukanisha.Labda ni kukosa ufahamu
lakini nashawishika kuamini ni UJUHA tu ndio unaweza kumfanya kijana
ambaye anatokwa na jasho mwili mzima kwa jua kali la mchana na yeye
anaaminishwa kuwa huo ni USIKU wa manane wenye baridi kali na anapaswa
kujifunika.,nae kama ZUZU akubali aseme NDIOMZEE ni usiku wa giza
totoro..
Siamini kuwa BAVICHA wanaamini kuwa CHADEMA yao
inaimarika.,siamini hivyo na nina uhakika kuwa hata HECHE haamini hivyo
labda ndio maana hajasema yeye kwa niaba ya Vijana, kamtafuta mmoja wa
wasiojielewa atoe salamu za bavicha kuwa sasa CHADEMA inaelekea
IKULU...vichekesho.
Ni CHADEMA ipi..? hii ambayo inaongozwa kifalme,
kibabe na kibedui..? Taasisi ambayo wachache tu ndio wana haki na
wengine ni wasindikizaji.? Chadema yenye Mwenyekiti asiye na Makamu,
Yenye Katibu Mkuu asiye na Naibu, Yenye Mwenyekiti wa Vijana asiye
naMakamu..? au Chadema ipi..? waswahili wanasema kinywa chenye mapengo
hakitafuni muwa.
Hivi IKULU ni Kariakoo sokoni, kuwa hata kwa
daladala au boda boda utafika..? nadhani wanaojiaminisha kuwa CHADEMA
ambayo viongozi wake wanajiuzulu mpaka vyombo vya habari vinapata
ukakasi kuripoti matukio hayo ya kujiuzulu eti ni Chadema inayoelekea
IKULU..chadema ambayo ilidharau wapinzani wengine na kuwakataa leo
wamerudi kuwapigia magoti waungane nao na kuwaomba msamaha kwa kauli
walizozitoa mwanzo za “ hakuna ndoa ya wanaume wengi” eti ndio CHADEMA
imara inayojiandaa kwenda Ikulu..?
CHADEMA yenye wazee kutoka kigoma
waliotembea kuja kumchukulia Fomu MBOWE,ambao sio kina MTEI, sio
KIMESERA bali ATHUMAN MZIGO al-maarufu“..MAPINDO SABA..” hajulikani
kokote kwenye siasa za Tanzania, mganga njaa ambae eti leo thamani yake
ni kubwa kuliko waasisi ambao bado wako hai akina MTEI..,eti yeye ndio
aamue nani anafaa kuendesha Chama hicho...off all people MAPINDO
SABA..??? kweli chadema kweli..,mapindo saba ndio awe muamuzi wa chadema
inayoelekea IKULU..seriously..???
Ikiwa MAPINDO SABA ndio Mzee wa
CHADEMA leo na MASONGA ndio kijana wa CHADEMA leo basi yatosha kusema
kuwa CHADEMA ya leo iko tayari kuelekea kuzimu sio Ikulu...
Naomba kuwasaidia Vijana wa BAVICHA Kufikiri.
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Josephine is passionate, dedicated, reliable, responsible, and hardworking. Team worker and able to face all challenging situations. Can ...
No comments:
Post a Comment