Songombingo la aina yake lilitokea leo majira ya saa 5 asubuhi makao makuu ya polisi likimhusisha mwenyekiti wa CHADEMA
Freman Aikaeli Mbowe
Freman Aikaeli Mbowe
| Mmoja wa wanachama ambaye alibishana na askari na kujikuta akipata kibano na baadae kuachiwa |
Mwenyekiti
wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE leo
amefanya shughuli za jiji la Dar es salaam kusimama kwa muda baada ya
kufika makao makuu ya polisi jijini akiwa na wanasheria wa chama huku
mamia ya wanachama wake wakiwa nyuma yake kutaka kujua kinachoendelea
hapo ikiwa ni kuitikia wito wa jeshi hilo waliomtaka kufika kwa maelezo
zaidi.

Baada
ya mh MBOWE kufika makao makuu ya polisi aliingia ndani na kuhojiwa
zaidi ya masaa manne na kisha mwanasheria wa chama hicho mh TUNDU LISSU
kutoka na kauli kuwa mwenyekiti huyo ametuhumiwa kuwa makosa ya
uchochezi aliyofanya juzi jumapili wakati akihutubia wanachama wake
ambapo alisema kuwa wataandamana na kufanya migomo nchi nzima kupinga
bunge la katiba linaloendelea.

Hata hivyo kwa taarifa ya TUNDU LISSU ni kuwa mh MBOWE ameachiwa kwa dhamana kwa ajili ya kusubiri kesi yake hiyo.

Hata hivyo mh MBOWE alionekana kufichwa sana kiasi cha kutokuwa rahisi kuonekana na wafuasi wake
Nje
ya ofisi za jeshi la polisi wananchi ambao ni wafuasi wa CHADEMA
walionekana kuwa na hamu ya kumwona mwenyekiti wao ambapo kwa mara
kadhaa walisikika wakiimba na kupiga kelele ambapo polisi walianza
kuwasukuma na kusogeza silaha zo karibu ili hali iwe shwari. Aidha mwanasheria Tundu Lissu aliwataka watu waondoke hapo ili
kuepusha vurugu zisizo na msingi

| Viongozi wa chama hicho walikuwepo kuhakikisha kuwa hali inakua shwari |
| Mh TUNDU LISSU akizungumza na wananchi pamoja na wanahabari ambao aliwataka kuondoka katika maeneo hayo ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kuwaharibia zaidi katika kesi hiyo |
No comments:
Post a Comment