12 October, 2014

ANGALIA PICHA MAAJABU YA DUNIA MSICHANA AAMUA KUJIOA MWENYEWE

Uvumilivu wa kusubiri mwanaume wa kuja kumpigia goti na kumuuliza ‘will you marry me?’, umemshinda mwanamke mmoja wa Uingereza, aliyeamua kuchukua uamuzi wa kujichumbia na kujioa mwenyewe!

Grace Gelder ambaye ni ‘mme na mke’ alijichumbia November, 2013 na baadae kujioa March, 2014 na kuamua kufanya sherehe ya harusi yake iliyohudhuriwa na wageni 50.


Na ule wakati wa ile hatua ya ‘you may now kiss the bride’ ulipowadia, Grace alijibusu kwenye kioo.
Mwanamke huyo alisema baada ya kuwa single kwa miaka 6 aliamua ku-fall in love na ‘yeye mwenyewe’ baada ya kuona hapati mtu wa kumpenda.

Mwanamke huyo alisema kuwa pia wimbo wa Björk song Isobel ambao una mstari unaosema ‘My name’s Isobel, married to myself’, nao ulimuhamasisha kutimiza azimio lake.

Source: Mirror

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...