12 October, 2014

UPDATES: HABARI ZAIDI KUHUSU YULE MWANAFUNZI ALIYEJICHOMA KISU TUMBONI BAADA YA KUMFUMANIA BOYFRIEND WAKE.


Mapenzi bhanaaaa....hatari sana! Hayana cha wewe mzuri, au una cheo, au una pesa, ama hauna...yaani yakikukamata utajuta so mtu akifikiaga maamuzi ya hivi usimcheke kabisa!!....Sawa na kumtukana mamba huku mto bado hujavuka. Huyu ni mwanafunzi aliefahamika kwa jina moja la Moza alie mwaka wa kwanza katika chuo cha Uhasibu TIA Mkoani Singida amenusurika kufa baada ya jaribio la kutaka kujiua kwa kujichoma na kisu kushindikana,tukio hilo limetokea jana baada mwanafunzi huyo kumfumania mpenzi wake wa kiume akiwa na mwanamke mwingine.....Sasa ni hivi huyu mwanafunzi akitoka hosptitali unaweza kumshauri vipi ili asirudie kufanya kitendo hicho??Maana huwezi kujua labda bado anayo dhamira ya kujimalizia......ila wanaume mnapata dhambi sana kwa Mungu dah! Hivi mwanaume akiwa na mwanamke mmoja itakuwaje?? Au ataonekana mshamba??....Yaani tangu jana niliwaza hili tukio mpaka basi...Daaaah ngachoka mtoto wa kichaga mie!!


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...