21 October, 2014

I WONDER HOW DIAMOND FEEL RIGHT NOW...I FEEL SORRY FOR HIM!

Kilele cha fiesta siku ya juzi tarehe 18 octoba 2014 Tanzania na dunia nzima kwa ujumla imeshuhudia msanii Ally Kiba akioyesha kuwa uchawi hauna nafasi kabisa kwenye muziki baada ya kumkalisha Diamond ambaye siku chache zilizopita alijinadi kupitia Clouds fm kuwa yupo tayari kumsaidia Ally Kiba kufanya nae collabo na sasa kibao kimemgeukia yeye ndiye atakayesaidiwa kufanya collabo.
MASHABIKI: Mashabiki walikuwa hawataki kusikia lolote zaidi ya Ally Kiba. Mashabiki wengine walienda mbali zaidi na kusema bora wasimuone T.I wao wanamtaka Ally Kiba tu.
DIAMOND AZOMEWA KAMA MBWA: kila akiimba mashabiki kila kona ya uwanja walikuwa wakimzomea Diamond huku wakitaka Ally Kiba arudi stejini. Mashabiki wasikika wakisema ''kiba kiba kiba kiba kiba'' huku wakimzomea Diamod ''buuuh buuuh buuuh''
Diamond apata wakati mgumu, Davido na Ney wa Mitego watumika kumbeba Diamond lakini mashabiki hawakuacha kumzomea.
DIAMOND ATAFUTA MCHAWI WAKE: Diamond huku akitapa tapa anahisi amechezewa mchezo na Clouds fm au Ally Kiba eti kwa kile anachokiita mafanikio yake, mashabiki wamjibu ''nani akuchukie wewe? kwa mafanikio yapi? kubadilisha wanawake au kutokumaliza nyumba? kama tunachukia mtu mwenye mafanikio wa kwanza angekuwa Mengi na Bakhresa sio mtu ka wewe''
Alizomewa Kikwete mwaka 2012 pamoja na Yoweri Museven chuo kikuu cha dar es salaam, who is Diamond bwana?
Msanii huyo aliyekulia Tandale na kufanya biashara ya kuuza mitumba na voucher, siku kadhaa zilizopita alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa Jiji la Mbeya halina hotel inayoendana na hadhi yake, baadhi ya mashabiki kutoka Mbeya pia waahidi kumzomea siku akienda Mbeya kwani kumuacha ni kumuendekeza ipo siku atasema hajaona hotel ya kulala Tanzania nzima/hajaona chakula cha kula Tanzania na hatimae atasema watanzania wote sio level yake.
Ukweli ni kwamba Diamond kwasasa hapendwi nchini Tanzania, si kwamba ni msanii mbaya ila sababu kubwa ni dharau zake na kiburi. Hivyo aashauriwa aache kusingizia watu. ''Waliomzomea ni watu waliotoka kwao na wakalipa pesa zao''
Nimeamini kuwa ''MBELE YA ALLY KIBA UCHAWI HAUNA NAFASI''

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...