![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSGZVpeOenJrbFfblcPaoC0Wyzw-Bb3-59qC59NB1E3RfXu0b0DXa-Hv4-AoHmGomfcavbyJ2JFXYqFrDNtyfjc7bxwzwJ2AyFQb2YjY5q7OAQ7QUcD1CqfzdnWJGc2iydRMoc2G6uhe9m/s1600-rw/mchungaji-1.jpg)
Askofu Boniface Kwangu
Waumini wa kanisa la Anglikana wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza walisimamisha kwa muda shughuli za ibada kanisani hapo baada ya kutokea vurugu kubwa.
Vurugu hizo zilitokea baada ya baadhi ya waumini hao kumtuhumu Askofu wa kanisa hilo Boniface Kwangu kwamba ni mmoja wa wafuasi wa kundi la Freemasons na hufanya kazi za kundi hilo!!
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo Shadrack Lazaro alitoa tamko la jinsi askofu wao anavyofanya kazi la kundi la freemasons, ndipo waumini walipomvamia na kumtoa nje kwa nguvu na kusababisha vurugu kubwa.
Muumini huyo alisema pamoja na sababu kadhaa za kumkataa Askofu huyo, pia hawaridhishwi na tabia yake ikiwemo ya kutaka kubomoa sakafu akidai kuna hirizi imefichwa na baadhi ya waumini wake kanisani hapo.
No comments:
Post a Comment