21 October, 2014

INASIKITISHA SANA JAMANI!!!

Baba na mama baada ya kurudi kazini pamoja wakakuta
BARUA iko mezani SEBULENI ikisema.... "Baba
na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma
ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke maana ni
mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi,
najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndo
nipo kidato cha kwanza..." Napenda
kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii
barua sipo nyumbani, nimetoroka maana
nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa
sababu mimi ni kijana mwenyewe umri wa miaka
14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya. Tangu
mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na
binti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa
miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye
chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani
sikuwa napata hela za kutosha ila sasa
nimeanza kushika noti za shilingi 10,000...
Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na
ninampenda sana, amenifundisha njia za
kutafuta hela. Amenipangia kazi ya kuuza
madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku
anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku
tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba
wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku
analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote
akija lazima awe naye chumbani kwa muda wa
masaa 3. Msiwe na hofu, nipo salama kabisa
na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu
kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao
kwa hiyo biashara inakwenda vizuri, Rachel
amekwenda kupima afya na amekutwa na
upungufu wa kinga mwilini, mara nyingi
namridhisha anapotaka kitu fulani, iwe kufanya
naye mazoezi ya viungo au kufanya naye
mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa
unatakiwa kuwa naye karibu, ila mimi pia sijihisi vizuri
maana kila saa nakohoa tu na sina uhakika
kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka
miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka
miwili iishe atakuwa ameshajifungua, na ni
furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi
wangu sina la kuongeza kwaherini Mungu
akipenda tutaonana. N.B: "Baba na mama, mimi
nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni home work ya mwalimu wa
kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya
kusisimua, naomba muiangalie kama kuna
makosa!"

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...