23 October, 2014

JELA YAMNYEMELEA DAVIDO


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeombwa kutoa amri ya kuwapeleka jela miezi sita Afisa Mtendaji Mkuu  wa Clouds Media Group, Prime Time Promotions na Adedeji Adeleke (Davido) kwa kukaidi amri ya mahakama.
Maombi hayo yaliwasilisha na Wakili  Peter Kibatala  chini ya hati ya dharura jana akiwawakikisha wateja wake ambao ni wadai katika kesi hiyo, M/S Times Radio FM na M/S Times Promotions na Entetainment Limited .
Kibatala anadai mahakama hiyo pia inaweza kuwaamuru kwenda jela kipindi chochote itakachoona kinafaa kwa sababu walikaidi amri ya mahakama iliyozuia Davido kupanda jukwaani katika Fiesta 2014.
Maombi hayo yaliambatana na hati ya kiapo iliyoapwa na Mtendaji Mkuu wa Times Radio FM, Rehure Richard Nyaulawa ambaye anadai kwamba Oktoba 17 mahakama hiyo ilitoa zuio kwa Davido kufanya onyesho.
Alidai pamoja na kwamba kulikuwa na amri hiyo ya mahakama iliyotolewa na Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, msanii huyo alitumbuiza katika Fiesta.
Davido anadaiwa kuingia mkataba wa kufanya onyesho Novemba mosi mwaka huu kwa udhamini wa M/S Times Radio FM

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...