17 October, 2014

KUTANA NA MAJERUHI WA AJALI YA LORI LA MAFUTA MBAGALA

 Baadhi ya majeruhi wa ajali ya moto wakiwa  wodini. MAJERUHI 9 kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya. Kamera ya chanzo cha habari hii ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia. Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi ambao aliwataja majina yao kuwa ni  Mathayo Danie (21) na Hamis Ally (35). Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.

GPL

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...