Kama video hii hapoo juu haitafunguka, tafadhali copy link hapo chini itakufungulia video:
https://www.facebook.com/video.php?v=774094389296075&set=vb.100000865627945&type=3&theater
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana October 21, 2014, mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga, na Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, walifunguka kuhusu kashfa za umri, kudanganya elimu, kuwa na mtoto, na mengine zinazomuandama mrembo huyo tangu atwae taji hilo. Zifuatazo ni kauli zao: (kama unataka kusikiliza badala ya kusoma, wasikiilize hapo chini.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania hana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’ – Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’ – Lundenga
Hashim Lundenga akionyesha cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, kushibitisha umri wake.
‘Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo’ – Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? Lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda’ – Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, akiondoka na mama yake Mariam, mara baada ya mkutano na waandishi wa habari
‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original’ – Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu’ – Lundenga
Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara’ -Sitti
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – Sitti
Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu, akiingia ndani ya gari linaloendeshwa na mama yake, kuondoka baada ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu skendo zilizokua zikimkabili
Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli’
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’
Baadhi ya waandishi walimuhoji Sitti juu ya cheti hicho ambacho kinaonesha kimetolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Uzamini (RITA), Septemba 9, mwaka huu, siku 32 tu kabla ya kutwaa taji hilo.
Baadhi ya waandishi walimuhoji Sitti juu ya cheti hicho ambacho kinaonesha kimetolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Uzamini (RITA), Septemba 9, mwaka huu, siku 32 tu kabla ya kutwaa taji hilo.
Swali ambalo lilitawala kwenye kikao hicho lilikuwa ni kwa nini cheti hicho kitoke ndani ya muda mfupi wakati anaonekana alikuwa akiishi nje ya nchi kwa muda mrefu, na kwamba huwezi kuishi nje ya nchi bila paspoti ambayo pia upatikanaji wake unatakiwa kuwa na cheti cha kuzaliwa alisema kilipotea!
Akaulizwa alitoa ripoti kituo gani cha polisi ili waandishi waende kuulizia, akagoma!
Mama yake Sitti alipotakiwa kutoa ushirikiano katika kuokoa jahazi la binti yake ambae alionekana kushindwa kuwashawishi waandishi wa habari alisema "naomba muulize yeye maana ndiye mshiriki wa Miss Tanzania, mimi sijawahi kushiriki hata siku moja na hapa nimekuja kumleta yeye tu, hivyo siwezi kuzungumza lolote juu ya hilo, kikao hiki kimeandaliwa na Miss Tanzania na si ukoo wa Mtemvu,” alisema mama huyo.
Sitti akizungumza na waandishi wa habari ndani ya Ukumbi wa Ngorongoro katika Hoteli ya JB Belmont, Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
Sitti katika pozi na mtoto anaedaiwa kuwa ni wa kwake
Pasipoti ya kusafiria ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
No comments:
Post a Comment