UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni! Mwanamke mmoja, mkazi wa Kitongoji cha Buriba, Kijiji cha Sirari wilayani Tarime, Mara aitwaye Bunyige Chacha (25) amepigwa mshale kwenye makalio na mumewe, Ghati Nyamarandi kisa kikidaiwa kuanzia kwenye pesa ya mahari na
.![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_v13kVqJkarYlSuh_ODvrPN701TuIrFpwg-IkiiWzLMe9v0mZXblVRMS8QWCklErZBYmuw7mAD3FxTkUFMKaFwcMl2KfmxefoJQDZDbDeQh2K21_7y1BBEVFPonrUb5-1-l28Zbs1MmlfW0FNpAjQjk3m0m2qb1l2xOihnQeBbQvv6DcJQcjlV7ogEs3X-6e_sUWEniaxSoBuE_P8ZXHBBV8s0rm7SXYRJAHDEPH13PItFc-eLsbmo-s0V040SudH-qibtzyw68rYabhSlZCy6TaOrqiPU9pv-HeK6Xrx7k4JrN3nIUloAx2vcd7VW4T6Jf2of256O0ZxWzWaWteraFo0Zw91fsUR273cH5KbzAZp_qpdCXyTS3nu-EoGnq1w=s0-d)
Ghati Bunyige akiwa amekaa kwenye benchi akisubiri huduma ya matibabu katika…
Ghati Bunyige akiwa amekaa kwenye benchi akisubiri huduma ya matibabu katika…
watoto! Akisimulia mkasa wake mzito uliompata Oktoba 5, mwaka huu majira ya jioni, mwanamke huyo alisema siku hiyo, mumewe alirudi na kumuuliza walipo watoto wao wawili (hakuwataja majina) ambao aliwaondoa nyumbani siku kadhaa nyuma bila kumwambia.
Akasema, alipomuuliza hivyo tu, ndipo mumewe akamjia juu na kumshambulia kwa matusi huku akisema watoto aliwapeleka kuuzwa eneo linaloitwa Nyumba Ntobu. “Mume wangu alifika nyumbani, nilipomuuliza watoto wako wapi ndipo akanifungia ndani ya chumba na kunishambulia kwa matusi.
“Kwa bahati nzuri nilibahatika kutoroka na kukimbilia kwa majirani lakini wakati nikivuka uzio wa mlango nilianguka, akapata nafasi, akanirushia mshale ulionichoma sehemu ya makalio, chini ya mguu wa kulia,”alisema mwanamke huyo
.
Mama huyo aliongeza kuwa, watoto wake wawili waliuzwa Nyumba Ntobu na baba huyo kuchukua mahari bila kumshirikisha mke suala ambalo lilizua mtafaruku ndani ya nyumba mwanamke akidai watoto wake kila siku.
“Kwanza mume wangu alimwachisha masomo binti yetu wa kwanza ambaye alikuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Sirari, akamuoza Nyumba Ntobu na kupokea mahari yeye.
“Baadaye akamwachisha masomo binti yetu wa pili aliyekuwa akisoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Nyamaraga, nchi jirani ya Kenya, akamwozesha hukohuko Nyumba Ntobu na akapokea mahari peke yake.
“Baadaye akamwachisha masomo binti yetu wa pili aliyekuwa akisoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Nyamaraga, nchi jirani ya Kenya, akamwozesha hukohuko Nyumba Ntobu na akapokea mahari peke yake.
“Baadaye nilikuja kugundua kuwa, alikuwa akipokea mahari kwa siri kwa sababu alitaka kulipia mahari ili na yeye aoe mke wa pili ambaye anaishi naye tayari, lakini ni mke wa mtu,” alisema mwanamke huyo.
No comments:
Post a Comment