23 October, 2014

OBAMA APONZWA NA BUSU ALILOMPIGA GIRLFRIEND WA MTU!

Rais Barack Obama wa USA, alikwenda kwenye jimbo lake la nyumbani, Illinois, kupiga kura. Wakati akipiga kura jijini Chicago, pembeni yake kulikuwa kuna mwanamke, naye akipiga kura.
Boyfriend wa dada huyo, akipita kwenda kupiga kura, akampiga mkwara rais Obama kiutani kwa kusema: “Mr President, please don’t touch my girfriend” (tafadhali usimguse mpenzi wangu)
Mwanamke huyo, ambaye alitaja jina lake kuwa ni Aia Cooper, na la boyfriend Mike Jones, alishtuka na kucheka, na kusema “did he just say that!?” asiamini alichosikia:
Tafsiri ya utani na maongezi yaliyoendelea
Obama, akimjibu Mike Jones: Sikuwa na mpango huo [wa kumgusa girlfriend huyo])
Maongezi yakaendelea kati ya Aia Cooper na rais Obama
Aia Cooper: Samahani, tafadhali muwie radhi [boyfriend]
Obama: Najua. Huu ni mfano wa mshikaji kukuumbua bila sababu yoyote; bila sababu yoyote kabisa
Aia Cooper: Nilijua tu atasema kitu cha kituko lakini sikujua ni nini atasema
Obama: Sasa utarudi nyumbani, ukiongea na rafiki zako….Anaitwa nani?[akiuliza jina la boyfriend]
Aia Cooper: Mike
Obama: [akiigiza atakachosema Aia Cooper kwa rafiki zake] “Yaani hata siamini! Mike ni mpumbavu kweli”
Aia Cooper: [akiendelea kucheka] Ni kweli kabisa
Obama: [Akiendelea kuigiza atakachosema Aia kwa rafiki zake] “Nilisikia aibu! Bahati nzuri rais alikua poa yani”
Aia Cooper: Yaani natetemeka sasa hivi
Obama: Ni poa tu, sio hatari
Walipomaliza kupiga kura, Obama akielekea kwa Aia akasema: “Nipe busu sasa, ili apate kitu cha kuongelea”
Baada ya kumbusu Aia shavuni Obama akaendelea: “Sasa ana wivu kweli kweli” huku akiwaaga watu na kuondoka kutoka kwenye kituo cha kupiga kura. Video ya kituko kizima hapa chini

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...