23 October, 2014

MGANGA WA JADI ANASWA NA BUNDUKI ZIKIWA ZIMEFUNGWA HIRIZI NA NGOZI YA MNYAMA - KAHAMA SHINYANGA


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mganga wa kienyeji bwana Mtabanzila Buyiyi (70)mkazi wa mtaa na kata ya Malunga wilayani Kahama kwa kosa la kukamatwa akiwa na bunduki mbili aina ya gobore zisizokuwa na namba zikiwa na hirizi akimiziliki kinyume cha sheria.

JoJoTheFighter blog inaarifiwa kuwa tukio hilo limetokea juzi saa tano na dakika 41 asubuhi wakati askari polisi wakiwa doria na msako katika kata ya Malunga wilayani Kahama na kufanikiwa kukamata bunduki mbili  aina ya gobore zisizokuwa na namba zikiwa zimefungwa hirizi na vipande vya ngozi ya mnyama asiyefahamika katika nyumba ya mganga huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus  Kamugisha amesema bunduki hizo zilikuwa zinamilikiwa kinyume cha sheria na zinadaiwa kutumika kufanya matukio ya uhalifu sehemu mbalimbali za mkoa wa Shinyanga.

Aidha amesema pia wanamshikilia mtoto wa mganga huyo bi Nyamisi Mtabanzila(40) kwa kosa la kuendesha shughuli za uganga na baba yake bila leseni!

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...