22 October, 2014

SIKIA ALICHOSEMA MAMA WEMA ATAKA MAHARI YA MIL.100 ILI DIAMOND AMUOE MWANAE....

Habari ya mjini hivi sasa ni Ndoa ya msataa wa Bongo, Wema Sepetu na Diamond Platnumz.
Habari zinaarifu kuwa ili Diamond Platnumz aweze kumuoa Wema Sepetu ni lazima atoe shilingi milioni mil. 100.
Habari hizi ni kwa mujibu wa gazeti moja la udaku lililotoka hivi karibuni ambapo liliripoti kuwa mama Wema sepetu anataka mahari ya milioni 90 na ushee ili binti yake huyo asiyechuja umaarufu awe mkwe wa mama Diamond.
Inadaiwa kuwa sherehe za birthday za Wema na Diamond zilizofanyika hivi karibuni na kugharimu pesa nyingi ndiyo zinadaiwa kumtia hamasa mama Wema na kutaka mahari hiyo kubwa kwa madai kuwa Diamond anazo pesa na hashindwi kutoa pesa hiyo ili kumuoa Wema ambaye umaarufu wao wote wawili ni mkubwa sana hapa Tanzaia huku umaarufu wa Diamond nje ya Tanzania ukiwa mkubwa zaidi kuliko wa Wema.

Hata hivyo habari zaidi zinadai kuwa Wema mwenyewe yupo tayari kuolewa hata bure na Diamond.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...