Msafiri wa anga alizua sintofahamu, baada ya kukohoa ndani ya ndege na kutania “I was in Africa. I have Ebola. You are all screwed [Nimetokea Africa, na nina Ebola. Wote mko matatani.]”
Abiria huyo alisema hicho wakati wako angani, kwenye ndege ya US Airways Flight 845, iliyokua ikisafiri kutoka Philadelphia, PA, USA kuelekea Punta Cana, Dominican Republic.
Mara baada ya kutua, ndege hiyo ilikuta kikosi cha maofisa wa afya wakiwa wamevaa suti za kujihami (hazmat suit) wakiisubiri. Maofisa hao waliingia kwenye ndege hiyo na kumshusha abiria huyo, huku akisema kuwa alikua anatania tu. “I was just kidding, I ain’t from Africa.” (Nilikua nafanya mzaha tu. Sijatokea Africa) alisema abiria huyo wakati akisindikizwa na maofisa hao.
“Tulipotua Punta Cana, flight attendant alitutangazia kuwa kuna Abiria aliyekuwa Africa hivi karibuni, na ana Ebola,” alisema abiria aliyerekodi video hii.
Ingawa ilithibitishwa baadae kuwa ilikua ni utani tu, maofisa na abiria wengi walikasirishwa na kitendo cha abiria huyo, na kusema suala la Ebola si la kulifanyia mzaha.
No comments:
Post a Comment