Pichani ni mti unaodaiwa kunyanyuka ghafla baada ya kuanguka miaka mitatu iliyopitakatika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma, iliyopo wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Katika hali ya kushangaza huku kila mtu akifikiria yake baada ya juzi huko mkoani Tabora, kutokea tukio la aina yake ambapo inaelezwa kuwa mti aina ya Msufi uliokuwa umeanguka yapata miaka mitatu iliyopita umesimama ghafla tena kwa sauti kubwa ya mrindimo na kuwafanya wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.
Tukio hilo limetokea Oktoba 17,mwaka huu,katika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma katika wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Inaelezwa kuwa mti huo wenye kipenyo cha futi 2 uliinuka na kuwa kama zamani baada ya kutokea upepo mkali katika kijiji hicho.

Wananchi walikusanyika kila mmoja akitaka kuchukua angalau gome la mti huo kwa ajili ya dawa ama kumbukumbu.
Mti huo ulioanguka na kuchomwa moto miaka 3 iliyo pita sasa wainuka na kusimama wananchi wakaamua kuukata na kuchukua vipande vya mti huo kwa imani za kishirikina {kizimba}.Na maajabu mengine yakatokea ulipomalizwa mti na kubaki shimo ndani ya shimo pakawa na vitu vya thamani kama pesa nyingi,pingu za mjerumani n.k. Vilivyotumiwa na watu wa zamani.Watu wakachukua na kufanya shimo hilo kubaki jeupe,na hapo ndipo shimo hilo lilipoamua kuanza kulia kama binadamu.
TIZAMA VIDEO HAPA CHINI.

No comments:
Post a Comment