Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi.
SERIKALI imetaja vijiwe vya wauzaji wa dawa za kulevya ‘unga’ vilivyopo katika mikoa mbalimbali nchini.
Pia,
imesema inafanya uchunguzi ili kubaini kama Watanzania waliokamatwa na
dawa za kulevya nchini China ni Watanzania kwa kuzaliwa au ni watu
waliotumia tu pasi za kusafiria (pasipoti) za Tanzania.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu hali ya dawa za kulevya hapa nchini.
Alisema ni
kweli kuna Watanzania zaidi ya 80, ambao wamekamatwa nje ya nchi kwa
kosa la kukutwa na dawa za kulevya. Lukuvi alisema kati yao, Watanzania
19 walikamatwa nchini China kwa kosa hilo la kukutwa na dawa za kulevya.
Alisema hivi sasa Serikali kwa kushirikiana na Balozi wa
Tanzania nchini China, inafanya uchunguzi ili kuona kama watuhumiwa hao
kweli ni Watanzania au wametumia pasi za kitanzania.
“Ni kweli
kuna watu ambao wamekamatwa nchini China na wanasema ni Watanzania, sasa
tunachofanya hivi sasa ni kuhakiki kama kweli hao ni Watanzania au
wanatumia pasi za Tanzania za kughushi huku wakiwa si watanzania,’’
alisema.
“Hata mimi kuna mtu kapigiwa simu kaambiwa nimepata
pancha njiani hivyo nahitaji fedha na alipotuma fedha akaona jina langu
limejitokeza na aka tuma wakati si kweli ni suala la kughushi hivyo
wanaweza kughushi hata pasi zetu,’’ alisema.
Alisema kati ya
Watanzania 80 waliokamatwa nje ya nchi, Watanzania 29 walikamatwa Hong
Kong, 27 Brazil, watano Kenya na 19 China. Lukuvi alisema Watanzania hao
walikamatwa kuanzia Januari hadi Desemba 2013.
Alisema baadhi
ya Watanzania hao, tayari wamehukumiwa vifungo na wengine wanasubiri
hukumu zao. Kwa mujibu wa Lukuvi, pia katika kipindi hicho walikamatwa
watuhumiwa wanane ambao ni raia wa Nigeria, Togo, Liberia na Sierra
Leone.
Lukuvi alisema kwa upande wa Tanzania, dawa hizo za
kulevya hutumika zaidi kwenye vijiwe mbalimbali nchini. Alisema vijiwe
maarufu ni Ngarenaro na Mianzini mkoani Arusha, Msamvu (Morogoro),
Hazina, Kituo Kikuu cha mabasi (Dodoma), Meko na Mbuyuni (Kilimanjaro).
Vijiwe
vingine ni Kirumba, Nyamagana na Mbita(Mwanza), Kwa Mama John, Mafiati
na Mwanjelwa (Mbeya), Vigaeni, Sinani na kituo cha mabasi (Mtwara),
Mwanga na Ujiji (Kigoma), Majengo, Kakora na Makaburini (Shinyanga),
Mtego wa Simba (Kahama) na Sahare, Deep Sea, kituo cha basi, Barabara ya
11 na 12 katika Jiji la Tanga.
Vijiwe vingine vinapatikana
kandokando ya barabara kuu zinazounganisha mikoa na vituovya mabasi na
magari makubwa ya mizigo.
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaanza vikao vyake tena leo mjini Dodoma, huku kukiwa na jitihada kubwa za kujaribu kuweka udh...
No comments:
Post a Comment