18 November, 2014

STORI YA UTAFITI MAONI WA WAGOMBEA URAIS 2015, JANUARI MAKAMBA AJIBIZANA NA MHARIRI WA GAZETI KATIKA MTANDAO

JANUARI MAKAMBA.

Gazeti la Mtanzania leo la Novemba 14 lililokuwa na kichwa cha habari kinachosomeka hivi; “.. Utafiti watibua wagombea urais 2015.. January aupinga, Zitto amwambia aache siasa.. Keissy ashangaa Wasira kutosomeka katika ripoti..”

JayMakamba
Kupitia mtandao wa Twitter, hiki ndicho kilichoandikwa na mhariri Absalom Kibanda na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba:

J. Makamba  : “ Unaelezeaje suala la gazeti lako kunukuu kinyume kabisa na mtu alivyosema? Umeambiwa.
A. Kibanda    : “ Nimeambiwa kaka. Badala ya kuandika JM kahoji wao wakaona umepinga utafiti.”
J. Makamba  : “ Si kweli. Na nimesema specifically sipingi. Heshima ndogo niliyobakiwa nayo na Mtanzania imeisha.”
A. Kibanda    : “ You judge the paper kwa kosa ambalo msingi wake ni kauli yako?! Worldwide media zinafanya makosa hayo ya tafsiri”
J. Makamba  : “ makosa yanatokea, ni kawaida na yanasameheka. Kupindisha makusudi kwa malengo mahsusi ni dhambi kwa wasomaji, tasnia na mhusika”
A. Kibanda    : “ Kaka unless silijui hilo. Siwezi kuruhusu gazeti naloongoza likuhujumu wewe au mwingine yeyote. Hata awe Membe anayenichukia”

JayMakamba IV
JayMaka Mwisho

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...