Safari hii ndiyo basi tena ! Pamoja na
kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na
simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia
kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo
pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy
lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu
‘ Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa
Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul
‘ Diamond Platnumz ’ .
Sexy lady wa Bongo Movies , Wema Isaac
Sepetu ‘ Beautiful Onyinye’ .
KUMBE NI MUDA MREFU TU
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni
rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya
kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini
kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili
wasishuke kisanaa .
SAFARI YA CHINA
Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache
zilizopita Wema au Madam kama anavyopenda
kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda
China kuchukua mzigo bila kumwambia ni
mzigo gani na kwamba huko aliambatana na
wanaume wanne, wawili wakiwa ni Martin
Kadinda na Petit Man .
KAMA MBWAI , IWE MBWAI
Ilidaiwa kwamba wanaume wengine wawili
wapo kwenye mabano , jambo ambalo Diamond
au Dangote kama anavyopenda kujiita ,
hakuliafiki suala hilo lakini Madam akasema
liwalo na liwe yaani kama ‘ mbwai iwe mbwai ’
hivyo akampuuza na kwenda zake China !
AHADI HEWA?
Chanzo hicho kilidai kwamba, kuna wakati
Madam alimuomba Dangote au Chibu ampe
fedha kwa ajili ya mtaji ambapo jamaa huyo
alikubali lakini siku zikawa zinayoyoma bila
dalili hivyo Wema akaona wa nini kama mtu
mwenyewe hawezi kumsaidia ?
ANAMTUMIA KIBIASHARA ?
Ilisemekana kwamba, baada ya kuona hali
hiyo , Wema alijiongeza na kuanza kukubaliana
na makelele mengi kuwa jamaa huyo
anamtumia kibiashara huku yeye akilamba
shoo na kupiga fedha ndefu ndani na nje ya
Bongo.
UBAHILI WAMPONZA DIAMOND
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ ubuyu ’
kwamba, tabia ya Diamond ya ubahili , nayo
imechangia kwa Wema kukaa pembeni kwani
jamaa huyo siyo mkataji wa mkwanja kama
ilivyokuwa kwa yule kigogo wa Wema ,
Clement .
“ Wewe unamuonaje Wema ? Yule mtoto bei
mbaya bwana. Matunzo yake si mchezo . Sasa
Dangote na ubahili wake ndiyo hivyo atamsikia
Madam kwenye bomba , ” kilisema chanzo
hicho.
Staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu
Abdul ‘ Diamond Platnumz ’ .
BMW LATAJWA
Chanzo hicho kilitiririka: “ Unalikumbuka lile
BMW (gari ) alilodaiwa Wema kapewa na
Kadinda siku ya bethidei yake? Unajua
Diamond alikuwa Marekani , sasa aliporudi
akataka kujua BMW imetoka wapi maana yeye
alitoa Murano , hapo ndipo moto ukawaka na
wakawa hawaivani tena . ”
BETHIDEI YA DIAMOND
Habari ziliendelea kupeperushwa kwamba siku
ya bethidei ya Diamond ambapo jamaa huyo
alizawadiwa BMW X 6 na uongozi wake wa
Wasafi, Wema alikwenda kwenye shughuli tu ili
kuonekana kwenye kamera.
Ilisemekana kwamba, ndiyo maana kwenye
shughuli hiyo Diamond ndiye aliyekuwa
akihaha kuhakikisha Wema hapati usumbufu
tofauti na Wema aliyekuwa anafuata tu
maelekezo ‘ kishingo upande’ kwani ndani
yake hakuna mapenzi tena .
UKIMYA WAPITA
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio lile
kulipita ukimya fulani huku kila mmoja akiishi
kwake tofauti na awali ambapo Diamond
alikuwa akijinasibu kuwa huwa analala
nyumbani kwa baby (Wema ) , Mtaa wa
Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.
DRAMA KWENYE BETHIDEI YA AUNTY EZEKIEL
Kwenye bethidei ya mwigizaji ambaye ni
shosti wa Wema , Aunty Ezekiel , Diamond
ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini
kwenye Mgahawa wa Rodizio uliopo Masaki
jijini Dar, huku kukiwa na taarifa kwamba
Madam asingekuwepo kwa kuwa alikuwa
safarini .
Wakati shughuli ikiendelea , Diamond
alionekana mwenye furaha akiwa na timu yake
lakini ghafla alipoibuka Wema upepo
ukabadilika .
Wema alipoingia ukumbini akitokea safarini
hata kabla ya kwenda nyumbani, alimpita
Diamond, akaenda kusalimiana na Aunty kisha
akaanza kuzunguka kwenye meza kusalimiana
na mtu mmojammoja, cha ajabu alipofika
upande aliokuwa ameketi Diamond na timu
yake, aliwaruka na kwenda moja kwa moja
kusalimiana na mwigizaji Jacqueline Wolper
Massawe.
BMW la Sexy lady wa Bongo Movies , Wema
Isaac Sepetu ‘ Beautiful Onyinye’ .
MINONG’ ONO KILA KONA
Ishu hiyo iliibua minong ’ ono kila kona ya
ukumbi huo na kuthibitisha zile tetesi kwamba
hawapo kwenye uhusiano mzuri . Wakati Wema
akifanya yake na Aunty , Diamond alipishana
naye kama hawajuani na kukimbilia kwenye
gari akiwa na timu yake tayari kwa kutimua .
‘ HUYU DEMU SIYO ’
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kwa nini
Diamond na ‘ kruu ’ yake waliacha sherehe
wakitaka kutimua , mmoja wa memba wa timu
yake ya Wasafi alisikika akisema ‘ huyu demu
siyo, hata ungekuwa wewe ingekuuma. Jambo
alilomtendea mshikaji siyo poa kabisa’ .
WEMA VIPI ?
Alipododoswa Wema juu ya kuzama kwake
ukumbini na kumfanya Diamond achomoke
bila ya kusalimiana alishindwa kutoa majibu ya
kina na kusema hakujua nini kilimkimbiza ila
yeye alikuwa pale kwa ajili bethidei ya Aunt na
si kingine .
DIAMOND ANASEMA ?
Alipofuatwa Diamond kuzungumzia juu ya
kutoka nduki baada ya Wema kuingia
ukumbini hapo, aliomba mwandishi wetu
amwache kwa maana kwamba ampotezee na
kuzama kwenye ndinga lake na kuondoka kwa
mbwembwe.
Hata kesho yake alipotafutwa kwenye simu
yake ya mkononi ili aweze kuzungumzia hilo
hakuonesha ushirikiano kwani simu yake ya
kiganjani haikupokelewa muda wote
alipopigiwa .
TUMETOKA MBALI
Penzi la Wema na Diamond limekuwa
likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha .
Wawili hao waliwahi kumwagana kipindi cha
nyuma kisha kurudiana Oktoba , mwaka jana .
Kabla ya kurudiana , kijiti cha penzi la Diamond
kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel
Mungilwa ‘ Penny’ huku cha Wema kikiwa kwa
yule kigogo wake , Clement .

No comments:
Post a Comment