03 November, 2014

SIRI NZITO YAFICHUKA , KUMBE VIJANA WALIOHUSIKA KUMPIGA JAJI WARIOBA WANATOKA CHUO CHA MWALIMU NYERERE NI BAADA KULIPWA FEDHA

  • HII  NI  AIBU  KWA WASOMI  WETU   WANAOSHINDWA  KUTUMIA  AKILI  KWA  KUENDEKEZA   TAMAA  ZISIZOKUWA  NA FAIDA  YOYOTE  MBELE  YA  JAMII
Vurugu mdahalo wavunjika
Habari zilizopatikana kwa baadhi ya vijana ndani ya ukumbi wa mdahalo, zinaeleza kuwa waliofanya vurugu waliahidiwa kulipwa fedha baada ya kazi hiyo na kwamba, mkakati huo ulifanywa siku moja kabla ukiwahusisha baadhi ya wanavyuo.
Baadhi ya wanafunzi waliohusika wanatoka vyuo vya Mwalimu Nyerere Kigamboni na Chuo cha Usimamizi wa Maji na Maendeleo.
Baadhi ya wanafunzi hao walitumiwa ujumbe wa kwenda kufanya vurugu na mtu mwenye namba za simu 0656 501317 aliyejisajili kwa jina la Valence Kisima.
Katika ujumbe wake, Kisima aliwaandikia aliokusudia wakafanye vurugu kwamba; “Kesho Jumapili kuna kongamano Ubungo Plaza, mda (Muda) ni saa sita, nauli ipo kwa mshiriki mpe taarifa na mwenzio.
Ujumbe mwingine wa Kisima ulieleza; “But asivae rangi ya chama kijani wala njano coz 2kio ili ni maalum sana ntawapa maelekezo kesho saa tano nikija ukumbini.
Waliyosema awali
Awali kabla ya vurugu kuanza, Warioba alisema Watanzania hawapaswi kujivunia takwimu ya asilimia 81 ya masuala yaliyoingizwa katika katiba iliyopendekezwa, kwa kile alichoeleza masuala muhimu yaliyokuwa na nafasi ya kuleta mabadiliko yamewekwa pembeni.
Alisema mengi ya mambo yaliyoingizwa katika katiba hiyo ni yale mazuri yaliyochukuliwa katika katiba ya sasa huku masuala ya msingi yaliyopendekezwa na wananchi yakiwa yameachwa kando.
Aliongeza moja ya jukumu la tume aliyokuwa akiiongoza ni pamoja na kuchukua mazuri ya katiba inayotumika sasa na maoni mengine ya wananchi, huku akisema masuala ya tunu za taifa zilizoachwa na bunge maalum ni muhimu kwa ajili ya mabadiliko.
Butiku, alisema watazunguka katika mikoa ya Mwanza Mbeya na nchi ya Zanzibar, kwa ajili ya kufanya midahalo kama iliyofanyika katika maeneo mengine chini.
Alisema mdahalo wa jana, unapaswa kutafsiriwa kuwa ni wa watanzania na si wa makundi kama ilivyokuwa awali.
Aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kujua kilichomo ndani ya katiba hiyo, japo bado haijasambazwa kwa kiasi kikubwa na kwamba, kwa sasa inapaswa kujadiliwa na wananchi na siyo makundi.
“Tunataka mtaani katiba hii ijadiliwe pasipo kumuogopa mtu, hakuna kusimamiwa na yeyote wala chama chochote, katiba hii ni yenu ili kesho na kesho kutwa usije kumlaumu mtu au kulaumiwa na mjukuu wako kwa uamuzi mtakaofikia baada ya kura ya maoni,” alisema Butiku.

Humphrey Pole pole, aliwaeleza wahudhuriaji kuwa katiba iliyopendekezwa inapaswa kuangaliwa kwa umakini na kwamba, wananchi kuipigia kura ya hapana siyo dhambi.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...