Unaweza ukadhani ni ndoto lakini hii ni habari ya kweli baada ya Hifadhi
ya jamii NSSF kutangaza uwezekano wa kujengwa daraja la kihistoria
zaidi litakalounganisha Dar es salaam na Zanzibar.
Uwepo wa daraja hilo unaweza kuwa ni neema kwa Watanzania wote na hata
nchi za jirani kwani itarahisisha shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa
asilimia kubwa kwa kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.
Gazeti la moja liliripoti
kuwa kwa sasa Shirika hilo lipo katika mazungumzo na wataalamu
mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari
ya Dar kwa upande wa Bara na Unguja kwa upande wa Visiwani.
Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo si
ndoto bali ni ukweli na tayari wameanza mazungumzo ya awali ili kutimiza
malengo yao.
Umbali kati ya Dar na Zanzibar ni kilimeta73.43 sawa na maili45.62 hivyo
kuwepo na mradi huo ni jambo linalowezekana kwani kuna madaraja marefu
zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.
Kwa sasa daraja refu zaidi duniani kote ni lile la Danyang-Kushan
lililopo nchini China ambalo lina umbali wa kilometa 165 sawa na
maili102.4 ambalo lilifunguliwa Juni mwaka2011
No comments:
Post a Comment