Baada
ya story ya yule msichana anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua
headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo
ambapo amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo baada ya
jana kumuomba samahani mtoto huyo.
Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye
kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto
Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake
kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.
Amesema anajiona mwenye
hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya
kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo alikuwa
akimpiga kama njia ya kumkanya.
Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.

No comments:
Post a Comment