21 December, 2014

SHEREHE ZA SHIWATA ZAHAIRISHWA!


 SHEREHE za miaka kumi ya kuanzishwa kwa Mtandao wa WAsanii Tanzania (SHIWATA)zilizokuwa zifanyike Desemba 25, jijini Dar es Salaam zimeahirishwa.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa kuahirishwa kwa sherehe hizo kumetokana na wanachama wengi ambao walitakiwa kukabidhiwa nyumba zao kuwa katika sherehe za Krismas nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kuahirishwa huko kumesababisha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga Veterani lililokuwa lichezwe Desemba 25 kwenye uwanja wa Azam, Charambe mpaka litakapotangazwa tena.

Mwenyekiti Taalib alisema sababu nyingine ya kuahirishwa kwa sherehe hizo ni kutokana na maombi ya mgeni rasmi ambaye hakumtaja kuwa yuko nje ya nchi kikazi ambaye aliomba ahudhurie tamasha hilo la kihistoria.

Nyumba ambazo zitakabidhiwa ni 38 ambazo zimejengwa na kukamilika ambako wanachama hao walichangia ujenzi kwa kutoa fedha kidogo kidogo kupitia benki na kuchangua aina ya nyumba anayoitaka kutokana na kiasi alizochangia.
Ili kuwapatia makazi ya bei nadfuu wanachama wake SHIWATA inajenga nyumba za sh. 631,000, sh. 1,500,000, sh. 3,800,000 na sh. 6,400,000 ambazo mwanachama anagaiwa kila mwezi Juni na Desemba kila mwaka..

Alisema katika makabidhiano hayo wamiliki wa nyumba hizo pia watakabidhiwa vyeti maalum vya kumaliki nyumba zao katika sherehe kubwa itakayofanyika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga. Mpaka sasa SHIWATA ina wanachama 8,000.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...