Kijana mmoja mwenye mienendo ya kustaajabisha nchini
Uingereza, alipiga simu kwa polisi baada ya kumchinja mwenzake mwenye umri wa
miaka 14 ambaye walifahamiana tu kupitia mtandao.
Kijana huyo alipigia polisi simu na kuwaambia kwamba
angependa waende nyumbani kwake huku wakiandamana na wataalamu wa uchunguzi wa
mauaji kwani alikuwa amemuua rafiki yake. .
Kijana huyo kwa jina Lewis Daynes mwenye umri wa miaka 19 ,
ametajwa na polisi kuwa kijana hatari, mhalifu ambaye anawahadaa wenzake na
kisha kuwadhuru.
Inaarifiwa ilikuwa mara ya kwanza kwa wawili hawa kukutana
uso kwa uso kwani suiku zote mawasiliano yao yalikuwa kupitia internet.
Daynes, alifungwa jela maisha baada ya kiupatikana na hatia ya kumuua Breck Bednar mwaja jana.
Daynes
kutoka Grays, Essex, alimwalika Bednar nyumbani kwake baada ya kujuana
tu kupitia internet akiwambia alitaka sana kumuona. Bedner alipowasili
nyumbani kwa Daynes, Daynes alimfunga mikono yake na kisha kumuua.
Mamake Bedner |
Taarifa
hii ya kijana huyo kuwapigia polisi simu na kuwaarifu kuhusu mauaji
aliyoyafanya, imeibuka hii leo siku moja baada ya hukumu kutolewa dhidi
yake.
'ninahitaji
polisi kuja nyumbani kwangu,'' alisema kijana huyo na alipoulizwa ikiwa
alikuwa anakiri kufanya mauaji akaseme, '' Ndio , ninakiri. ''
Baadaye
aliwapa polisi taarifa zake, jina lake na alikoishi na kisha
kuwashukuru. Alidai kwamba alimuua rafiki yake Breck baada ya kumtisha
kwa kisu.
''Sikumbuki kilichotokea lakini nilimchinja, '' aliwaambia polisi.
Baadaye polisi walifika nyumbani kwake na kumpata Daynes akiwa mtulivu huku mwili wa rafiki yake ukiwa sakafuni.
Mamake Bedner amesema vijana wanapaswa kutahadhari wanapojihusisha na maswala ya mitandao
Daynes,
ametajwa kama kijana ambaye hakueleweka kitabia ila alipenda sana
kutumia muda wake kwenye kompiuta. Wazazi wake waliachana hali
iliyosababisha maafisa wanaoshughulika maslahi ya watoto kumpeleka kwa
familia ambayo sio yake ili aweze kutuzwa.
Alikatakata
nguo alizokuwa amezivaa akijaribu kuharibu komputa aliyokuwa anaitumia
ili kufuta ushahidi wa mazungumzo waliyokuwa nayo na rafiki yake kabla
ya kumuua.
Kabla
ya kuwapigia polisi simu, alimtumia mtu mmoja picha ya mwili wa Bednar
ushahidi wake kwamba amemuua. Hata hivyo polisi wangali wanachungaza
kumtambua mtu huyo.
Mamake
kijana aliyeuawa amesema anatuami kuwa kisa cha mwanake kitakuwa funzo
kwa vijana wanaojihusisha na michezo ya kwenye internet.
No comments:
Post a Comment