Mwanablogu nchini Saudia (PICHANI) amechapwa viboko hadharani kwa madai ya kutusi dini ya kiislamu.
Raif
Badawi ambaye alianzisha mtandao kwa jina ''Liberal Saudi Network''
alihukumiwa kifungo cha miaka 10 msimu wa joto uliopita.
Mahakama pia iliagiza acharazwe viboko 1000.
Amechapwa viboko hivyo katika mji wa Jeddah.
Ilieleweka kwamba angetandikwa viboko hamsini na kwamba alitarajiwa kuchapwa viboko zaidi wiki zilizofuatia.
Mwanablogu
huyo alichapwa viboko licha ya wizara ya maswala ya kigeni nchini
Marekani kutaka kuondolewa kwa adhabu hiyo walioitaja kama ya kikatili.
Via>>BBC
No comments:
Post a Comment