15 January, 2015

HUDUMA YA AFYA ANGANI YAZINDULIWA KENYA!


Kenya imezindua huduma yao ya kwanza ya gari la wagonjwa la angani  itakayosaidia kuwahamisha majeshi ya usalama waliojeruhiwa kwenye  mapambano.    Rais Uhuru Kenyatta alisema huduma hiyo ni muhimu kuhakikisha wanapata  tiba haraka.  Huduma hiyo inatarajiwa kuwapa matumaini zaidi wafanyakazi wa masuala ya  usalama wanaokabiliwa na vitisho vya mara kwa mara.  Baadhi ya wanajeshi na polisi wametoka damu mpaka kufa au kufa kutokana  na ukosefu wa maji maeneo ya vijijini nchini Kenya kwasababu ya muda  mrefu unaotumika kuwafikisha hospitalini.  Serikali ya nchi hiyo sasa imefanya makubaliano na Shirika la Msalaba  Mwekundu, Red Cross na kampuni binafsi ya madaktari wasio na mipaka ya  AMREF kutoa huduma za helikopta na magari wanapopata tu simu za kuhitaji  huduma hiyo haraka.   Huduma hiyo pia itatolewa kwa wafanyakazi wa serikali, hasa wale  wanaofanya kazi kwenye nyanja ya usalama vijijini na walio na vifaa  vichache vya kutolea matibabu.  Kundi la Kisomali la al-Shabab limeongeza mashambulio nchini Kenya  katika miaka ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...