Dawasco inawatangazia
wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa
kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za
Ijumaa na Jumamosi ya tarehe 23 na 24 Januari 2015, kuanzia saa kumi na
mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd)
kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (Cross-connection) ndani ya
Mtambo wa Ruvu Chini, Bagamoyo.
Kuzimwa kwa mtambo wa
Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; Mji wa Bagamoyo,
Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach
na Kawe.
Maeneo mengine ni
Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo,
Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City
Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa
Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.
Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
Au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja namba 022- 2194800
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment