MASHABIKI
wa Majimaji ya Songea juzi walijikuta katika wakati mgumu pale
waliposhambuliwa na askari Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia na
baadhi yao wakilazwa hospitali ya mkoa wa Ruvuma(HOMSO) wodi ya majeruhi
wakitibiwa baada ya majeraha ya kipigo kutoka kwa askari.
Askari hao ambao walionekana kutumia nguvu
zaidi kuliko mashabiki ambao waliokuwepo kiwanjani hapo, baada ya
kumalizika kwa mchezo wa ligi Daraja la kwanza (FDL) kati ya Majimaji
na Kurugenzi ya Mufindi, mchezo ambao ulimalizika kwa timu hizo
kufungana bao 1-1, mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa Majimaji
mjini hapa.
Katika
mchezo huo Majimaji ndio walikuwa wakwanza kujipatia bao la kuongoza
katika dakika ya 12 na Ditram Nchimbi kwa mpira wa kichwa, kabla ya
Kurugenzi kusawazisha bao hilo katika 54 Asili Mkondya aliyeingia
kuchukua nafasi ya Stanley Msangila, na Majimaji walikuwa wakicheza
mbele ya Mkufunzi wao wa kiufundi na Mkurugenzi wa kituo cha michezo cha
Symbion cha jijini Dar es Salaam, Stuward Hall.
Pamoja
na mashabiki wa Majimaji kulalamika kuwa mashabiki wa Kurugenzi
wamekuwa na tabia ya kuzishambulia timu pinzani zinapocheza kwenye
uwanja wao wa nyumbani kwa kushirikiana na askari polisi wa wilaya
hiyo, kitu ambacho askari wa kikosi hicho wakahisi huenda mashabiki hao
wakalipiza kisasi wanachokifanya mashabiki wenzao wa timu pinzani.
Polisi
walianza kurusha mabomu baada ya mashabiki wa Majimaji kumzomea
Mbunge wao, Emmanuel Nchimbi wakati akitoka uwanjani kushuhudia
mchezo huo, baada ya Mbunge huyo kuwapungia mkono mashabiki hao
akiwataka watulie,huku mashabiki wao walijibu hatukutaki tuachie
tuwafunze adabu hao Kurugenzi , kauli ambayo ilionekana iliwaudhi
Polisi na kuanza kutumia nguvu kupiga mabomo na kutembeza kipigo
pasipo sababu ya kimsingi kama kwa binadamu mwenye akili mwenye utashi
wa kutambua baya na zuri.
wachezaji wa kurugenzi wakitolewa uwanjani kwa gari la polisi |
Pamoja
na Polisi kuwaondosha uwanjani wachezaji wa Kurugenzi na viongozi wao
salama bado waliendelea kutengeneza chuki kwa wananchi kwa kuendelea
kuwashambulia, kwani askari hao walihama ndani ya uwanja wa Majimaji na
kuhamia mitaani kupiga wananchi wasiokuwa na makosa kama soko la
Manzese ambapo waliingia na kuanza kuwashambulia wafanyabiashara pamoja
na wanunuzi ambao waliingia katika soko hilo kutafuta mahitaji yao.
Baadhi
ya mashuhuda wetu ambao walikuwa wakifuatilia unyama wa askari hao
alidai hasira za askari hao zilimalizika maeneo ya Bombambili umbali
wa kilometa mbili kutoka ulipo uwanja wa Majimaji ambapo walipiga
mabomo na kuwashambulia wananchi wasiokuwa na hatia na kurejea kambini
kwao, huku wakiwaacha wananchi wa Songea katika mshangao mkubwa juu ya
hatima ya chombo chao kilichopewa dhamana ya kulinda usalama wa maisha
ya raia na mali zao.
Mmoja
wa wahanga hao pamoja na mwandishi wa mtandao wa www.jamvila habari.com
alijikuta katika wakati mgumu pale alipolazimishwa kulala chini
kifudifudi huku askari mmoja akimlinda kwa kumwekea bunduki ya aina ya
SMG kisogoni wakimzuhia asipige picha za tukio hilo jinsi linavyoendelea
pamoja na kumpa vitisho wangeweza kuondosha uhai wake mara moja, alidai
alitii amri hiyo kwa lengo la kuokoa uhai wa maisha yake.
Mwandishi
wa gazeti pia aliweza kupata bahati na kuzungumza na baadhi ya
majeruhi ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa(HOMSO) wakipatiwa
matibabu akiwemo mtangazaji wa kituo cha Radio cha mjini hapo (Jogoo Fm)
ambaye amelazwa wodi namba mbili kitanda namba tatu, Hossam Ulaya
alidai alishambuliwa na askari saba wa kikosi hicho wakati akijaribu
kuwasalimisha wachezaji wa timu ya mkoa ya wanawake, baada ya Polisi
kuwatembezea kichapo kisichokuwa na sababu, huku mmoja ya kati ya hao
wachezaji amelazwa wodi namba tano ambaye amejitambulisha kwa jina la
Arasha Chande
Mtangazi
huyo alisema kichapo hicho kilimkuta baada ya kuona wachezaji hao wa
timu ya mkoa ya wanawake wakichalazwa bakora na askari ambao
wakiongozwa na mkuu wa kituo cha Polisi cha wilaya ya Songea, ambaye
alimtaja kwa jina moja la Mashimbi ambaye alikwenda kwa ajili ya
kuwasalimisha wachezaji hao, wakati huo anakwenda kuwasalimisha akiwa
amefuatana na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la mpira wa
miguu nchini(TFF), James Mhagama.
Alisema
pamoja na kichapo hicho bado aliweza kumshuhudia mjamzito
wakimshambulia kwa marungu katika maeneo mbalimbali ya mwili wake huku
akilia kwa maumivu na kumtaja askari mmoja wa kike ambaye na alikuwa
akishiriki unyama huo alidai aliweza kunukuru jina moja la Jojina, na
baadaye askari huo alikwenda na kuanza kumfariji kwa kumpa pole wakati
wamemuumiza.
Alisema
askari hao pamoja na vitendo vya vya kinyama kubwa zaidi alidai
waliweza kumvamia mtoto wa jinsia ya kiume ambaye alidai anaweza kuwa na
umri wa miaka saba kwa kumshambulia kwa marungu, mateke na kupelekea
kumsababishia maumivu , alidai licha ya mtoto huo kuangua kilio askari
hao waliendelea kumpa kichapo aliokolewa na kikundi cha vijana ambao
walijitoa muhanga kwa kuwavamia askari hao kwa kuwarushia mawe na
kuamua kumuacha na kukimbia huku mtoto huyo akiwa tayari amepoteza fahamu
Hata
hivyo habari za kitelejensia ambazo zimenaswa na gazeti hili huenda
vita hiyo ikaendelea Januari 24 mwaka huu, wakati Mlale JKT
watakapokutana na Kurugenzi ya Mufindi katika mchezo wa ligi hiyo ya FDL
ambao utakuwa wa kulipiza kisasi kati ya wananchi na jeshi la Polisi
ambapo wananchi wanajipanga kwa mashambulizi, gazeti hili litaendelea
kuwapatia nini kinachojili juu ya tukio hilo ambalo linahisiwa huenda
likapelekea kutokea kwa mauaji.
Na
baadhi ya wadau wa soka wa Songea walizungumza na gazeti hili wengi
wao wamelitupia lawama jeshi la Polisi wamekuwa wakitumia nguvu nyingi
kulikoni akili na maharifa, huku wakidai hata nchi ikiingia kwenye
machafuko yatakuwa yanasababisha na askari wa jeshi la Polisi na si
jeshi la wananchi, kwani michezo ujenga umoja mshikamano wa kindugu na
pia inaendeleza kudumisha amani na utulivu wetu tulionao Watanzania
kwa sasa huku wakidai Serikali wanatakiwa walione hilo.
Hata
hivyo Katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma (FARU) Ahamed Challe
amesikitishwa na maamuzi ya jeshi la Polisi la kutumia nguvu kuliko
akili, alidai ilikuwa haina sababu ya kuwashambulia wananchi na
kuwajeruhi wakati wachezaji wa kurugenzi walikuwa wamewaondoa uwanja
wakiwa chini ya ulinzi wao kwa amani na utulivu, baada ya hapo nao
wangeondoka na wangeendelea na majukumu yao mengine ya kiusalama badala
ya kuingia mitaani na kuanza kuwashambulia wananchi bila ya sababu.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikheli
hakuweza kupatikana kuelezea tukio hilo lakini ameweza kunukuliwa
wakati akiingia hospitali ya mkoa, kumtakia hali huyo mtangazaji wa
kituo cha Jogoo Fm, Hossam Ulaya kuwa taarifa
alizozipata kutoka kwa maofisa wake walidai wananchi walikuwa na lengo
la kuwafungia milango askari wake ndani ya uwanja wa Majimaji kwa lengo
la kuwashambulia, kitu ambacho si kweli huo ni uongo mtupu wanania ya
kujitetea mbele ya Kamanda wao.
No comments:
Post a Comment